Home Mchanganyiko RC NDIKILO -WAKULIMA NA WAFUGAJI TUMIENI BONDE LA MTO RUVU KWA KUFUATA...

RC NDIKILO -WAKULIMA NA WAFUGAJI TUMIENI BONDE LA MTO RUVU KWA KUFUATA SHERIA NA MUUCHE KUBUGHUDHIANA

0

****************************

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
SERIKALI Mkoani Pwani ,imeelekeza wakulima na wafugaji watumie bonde la mto Ruvu kwa kuheshimiana na kufuata sheria pasipo kundi lolote kuwa kero ya mwingine ,na kusisitiza ni bonde muhimu kwa jamii zote hizo .
Aidha serikali Mkoani hapo imewaasa wakuu wa wilaya ,maafisa tarafa,wakurugenzi na wataalamu mbalimbali,kwenda kwa wananchi kujua changamoto na kero ambazo bado ni kilio kwao ili kuzitafutia ufumbufu badala ya kusubiri kupelekewa kero ofisini ama wananchi kuzifikisha ngazi za juu .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alitoa rai hizo wakati alipofanya kikao cha kazi ,kujichimbia na Wakuu wa Wilaya kuweka Mikakati ya kutatua Kero za Wananchi, Migogoro ya Ardhi na  kutathimini Miradi ya Maendeleo Mkoani humo .
Alieleza ,serikali ya mkoa haijawahi kutamka jamii moja iondoke katika bonde hilo, bali inasisitiza kuishi kwa amani na kuheshimiana bila kuingiliana kwenye majukumu yao na kundi moja kulia kutokana na kundi jingine kumsababishia hasara .
Ndikilo alisema ,bonde hilo lina ardhi yenye rutuba,malisho na maji na inafaa kwa makundi yote .
“Wakulima msizibe njia za mifugo kwenda katika malisho na maji na ,wafugaji wasilishe katika mashamba ya wakulima na kutia hasara wakulima kulishwa mazao yao ;:”
Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani alibainisha ,kwasasa serikali itaendelea kuchukua hatua kwa mfugaji ama mkulima ambae atakwenda kinyume na sheria zilizopo .
“Na ndio maana Ranchi ya Ruvu imetengwa ardhi hekari 40,000 itakayogawiwa vitalu kwa ajili ya wafugaji wenye makundi makubwa ya mifugo ” hii itasaidia kupunguza ufugaji holela “;alisisitiza Ndikilo .
Nawataka wafugaji wenye mifugo mikubwa kwenda kuchukua vitalu hivyo kwa bei nafuu iliyopangwa .
Hata hivyo ,aliwataka viongozi mbalimbali na wakuu wa wilaya na kata kusimamia miradi ya maendeleo ,na kuhakikisha inajengwa kwa wakati na kuzingatia viwango .
” Tuwafuate wananchi walipo kujua kero zao ,kuna migogoro ya ardhi,matatizo ya maji,barabara nyingine mbovu hazipitiki ,kero zote hizi ni wajibu wetu kuzitatua.
Ndikilo alisema kwamba ,wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wameteuliwa kumsimamia ngazi ya mkoa na wilaya ,endapo wakiyumba na kushindwa kutimiza wajibu huo wanamuangusha ,kwani Rais John Magufuli ameshakuwa mfano katika utendaji kazi wake na kasi ya kuinua maendeleo na uchumi wa nchi.
Wakati huo huo ,meneja wa Ranchi ya Ruvu, Elisa Binamungu ,alifafanua wametenga eneo la hekta 20,000 ambalo limepimwa vipande vya hekta 500 na kupatikana vitalu 40 vinavyotumika kwa wafugaji wadogo ili kupunguza mifugo holela mkoani hapo .
Anaeleza ,wanahamasisha kuanzia ngazi ya kijiji ,kata lengo mifugo inayoingia ndani ya Ranchi iingie kwa utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na kila heka moja mfugaji anailipia sh. 3,500 kama tozo kwa mwaka.
Kikao hicho pia kilihusisha kamati ya Usalama Mkoa na Wakuu wa Taasisi za Serikali Mkoani Pwani.