Home Mchanganyiko RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA HABARI UTALII NA...

RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA HABARI UTALII NA MAMBO YA KALE ZANZIBAR

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha Kitabu cha Maelezo ya Maeneo ya Historia ya Zanzibar, baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar (kulia kwa Rais) Mhe. Mahmoud Thabit Kombo,wakati wa Kikao cha Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwaka
2020/2021,kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanziba, na (kushoto  kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii  na Mambo ya Kale  Bi. Khadija Bakari Juma. Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Habari Dkt. Saleh Yussuf Mnemo na Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Utalii na Mambo ya Kale Dkt. Amina Ameir Issa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanziba,kupitia Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Wizara hiyo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mahmoud Thabit Kombo

WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwasilisha Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake kwa Kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, kikiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) na (kushoto kwa Waziri) Katibu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu
Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na (kulia kwa Waziri) Mshauri wa Rais
Masuala ya Historia a Mambo ya Kale Mhe. Ali Mzee Ali.

WAKUU wa Idara mbalimbali za Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakifuatilia Kikao cha Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yao kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Wakati Katibu Mkuu Bi. Khadija Bakar Juma, akiwasilisha taarifa ya Mpoango Kazi, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Bi. Khadija Bakari Juma akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji Mpango Kazi wa Wizara yake kwa kipindi cha mwaka wa Fedha 2020/2021, kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Utalii na Mambo ya Kale  Dkt.Amina Ameir
Issa na Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Habari Dkt. Saleh Yuusef Mnemo.

MSHAURI wa Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akizungumza wakati wa Kikao cha Utekelezaji Mpango Kazi kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kikiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kushoto Mshauri wa Raius Pemba Mhe.Dkt. Maua Abeid Daftari, Mshauri wa Rais Masuala ya Historia na Mambo ya Kale Mhe. Ali Mzee Ali
na Waziri wa Utali Habari na Mambo ya Kale Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.(Picha na Ikulu)