Mgombea wa Urais ,John Shibuda akikabidhiwa Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADA-TADEA katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Mgombea wa Urais ,John Shibuda wakionyesha Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADA-TADEA katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 pamoja na Mgombea Mwenza Hassan Kijogoo mara baada ya kuchukua Fomu hizo katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma.
Mgombea wa Urais ,John Shibuda kupitia Chama cha ADA-TADEA katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 akisaini Kitabu mara baada ya kuchukua Fomu hizo za Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma
Mgombea Mwenza kupitia Chama cha ADA-TADEA Hassan Kijogoo akisaini kitabu katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma.
Mgombea wa Urais ,John Shibuda wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADA-TADEA katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 akiagana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma mara baada ya kuchukua Fomu.