Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtunuku Tuzo Maalum Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kwa kutambua mchango wake na kuwawakilisha Wanawake Vizuri katika majukumu yake, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jijini Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………………………………………………………….
Na. Alex Sonna,Dodoma
Baraza Kuu la Umoja wa wanawake Tanzania la Chama Cha Mapunduzi(UWT) limetakiwa kufanya mchujo wa wagombea kwa haki bila kumuonea mtu hayaa, endapo wakishindwa kufanya hivyo vikao vya juu vya chama vitafanya vitaamua.
Wito huo umetolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan Wakati akifungua Bazara hilo ambalo ni maalum kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge wa viti maalum waliopitishwa kwenye kura za maoni kwenye mikoa jijini Dodoma..
“Baadhi ya maeneo kumetokea kasoro kadhaa za uchaguzi hivyo sasa ni wakati sahihi wa Baraza hili kusahihisha changamoto na ukiukwaji wa taratibu uliyotokea kwa kufanya mchujo wa haki bila kumuonea mtu aibu au hayaa”ameeleza Samia.
Aidha Samia ameeleza kuwa adhima ya kutaka kauli hiyo kutendewa haki ni kupata watu watakoa peperusha bendera ya chama katika Uchaguzi Mkuu ili kuwa na viongozi bora na waadilifu.
“Lengo letu sisi kama chama ni kuhakikisha viongozi watakaokiwakilisha chama chetu ni waadilifu, wachapakazi na wenye kuendana na maadili ya chama na dhima yetu ya Hapa Kazi Tu “, amesisitiza Samia.
Aidha Mhe.Samia amesema kuwa kiongozi mzuri ni yule aliye na uwezo wa kuongoza wenzie kwa kujiamini na kushirikisha wengine na siyo mtoa rushwa au mpokea rushwa.
Katika hatua nyingine Samia amewataka wanawake wote wa CCM kujiandaa na kujipanga kwa uchaguzi wa dola ili kuhakikisha CCM inashinda kwa ushindi mkubwa.
Naye Mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudencia Kabaka, ametoa rai kwa wanawake hao kuhakikisha wanakuwa wamoja ili kukamilisha dhana ya mafiga matatu katika sanduku la kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.