Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya katika kikao cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha Mwaka 2020/2021 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 10/08/2020. Viongozi katika Wizara ya Afya zanzibar wakiwa katika Kikao cha Utekelezaji Mpango kazi wa Mwaka 2020/2021 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).[Picha na Ikulu] 10/08/2020. Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee alipokuwa akichangia katika Kikao cha Utekelezaji Mpango kazi wa Mwaka 2020/2021- kulichofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar, (kushoto) Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Mhe. Juma Makungu Juma,[Picha na Ikulu] 10/08/2020. Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao katika Kikao cha Utekelezaji Mpango kazi wa Mwaka 2020/2021 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 10/08/2020. Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati wakiwa katika Kikao cha Utekelezaji Mpango kazi wa Mwaka 2020/2021 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).[Picha na Ikulu] 10/08/2020. Mshauri wa Rais Pemba Dk.Mauwa Daftari akichangia katika kikao cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha Mwaka 2020/2021 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.] 10/08/2020. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Nd,Halima Maulid Salum alipokuwa akisoma taarifa ya Mpango kazi wa Wizara hiyo kwa mwaka 2020/2021 katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Mkurugenzi Mkuu katika Wizara ya Afya Dk.jamala Adam Taib (kulia).[Picha na Ikulu] 10/08/2020.