Home Mchanganyiko “WATANZANIA WANAFAHAMU NA KUMILIKI MAFANIKIO YA SEKTA YA AFYA YA MSINGI CHINI...

“WATANZANIA WANAFAHAMU NA KUMILIKI MAFANIKIO YA SEKTA YA AFYA YA MSINGI CHINI YA MIAKA MITANO ILIYOPITA“ DKT. GWAJIMA

0

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Asunga akimkabidhi Naibu Katibu  Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima zawadi ya kikombe baada ya TAMISEMI kushinda nafasi ya Tatu katika nafasi ya Wizara zilizofanya vizuri katika maadhimisho ya 28 ya Sikukuu za Nanenane 2020 yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Naibu Katibu  Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa na Mratibu wa Maonesho ya Nanenane kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Yusuf Semuguguruka wameshikilia zawadi ya kikombe  walichopata TAMISEMI baada ya kushinda nafasi ya Tatu katika nafasi ya Wizara zilizofanya vizuri katika maadhimisho ya 28 ya Sikukuu za Nanenane 2020 yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Naibu Katibu  Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima (kwanza kulia), Mratibu wa Maonesho ya Nanenane kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Yusuf Semuguguruka (pili kutoka kushoto) na baadhi ya watumishi wa TAMISEMI wakiwa wameshika zawadi kikombe  walichopata TAMISEMI baada ya kushinda nafasi ya Tatu katika nafasi ya Wizara zilizofanya vizuri katika maadhimisho ya 28 ya Sikukuu za Nanenane 2020 yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Naibu Katibu  Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa maonesho ya nane nane 2020 na Mratibu wa Maonesho ya Nanenane kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Yusuf Semuguguruka  katika maadhimisho ya 28 ya Sikukuu za Nanenane 2020 yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Naibu Katibu  Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja na watumishi walioko katika Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi  katika maadhimisho ya 28 ya Sikukuu za Nanenane 2020 yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

……………………………………………………………….

Na. Majid Abdukarim, Simiyu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imeshika nafasi ya Tatu katika nafasi ya Wizara zilizofanya vizuri katika maadhimisho ya 28 ya Sikukuu za Nanenane 2020  na kuibuka na zawadi ya kikombe katika kilele cha maonesho hayo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu  Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima jana  katika kilele cha maonesho ya 28 ya Siku ya NaneNane yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Aidha Dkt. Gwajima ametumia kilele hicho cha maadhimisho hayo kuwaasa watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa kutekeleza kwa weledi na ufasaha wajibu wao katika kuwatumikia watanzania ili waweze kutumia muda wao mwingi kujishughulisha na maendeleo ya kiuchumi na siyo kufuatilia ufumbuzi wa kero zao zinazozuilika.

“Ofisi ya Rais TAMISEMI imesogezwa katika viganja vyenu Wananchi kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano hivyo ni vyema Watanzania mkatumia fursa hiyo kwa kupiga namba 026 2160310 na kuwasilisha shida au kero zenu kwenye kituo chetu cha huduma kwa wateja hatua itakayowasaidia kuepuka gharama za safari zisizo za lazima kuja Dodoma kufuatilia jambo ambalo ufumbuzi wake ungepatikana kwa kuzungumza tu kupitia huduma hii”ameelezaDkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amesema kuwa niimani yake kama watanzania watatumia namba hiyo ipasavyo  basi itasaidia katika kulinda na kukuza uchumi wa kati kwani hawatapoteza muda wala fedha kugharamia safari za kwenda Dodoma kufuata huduma ambayo imesogezwa kiganjani kwake bali atapata ufumbuzi na mara moja kurejea kwenye utekelezaji wa majukumu yake ya kujenga familia naTaifa.

Pia Dkt. Gwajima ameeleza kwa ufasaha majukumu yaTAMISEMI kwamba kwa ufupi ni yamejikita katika kuimarisha ushirikishwaji wa Wananchi wenyewe  wa weze kutekeleza mipango yao inayogusa maisha yao ya kila siku  ikiwemo huduma za jamii zaAfya, Elimu na Miundombinu katika maeneo yao Ufuatiliaji na uratibu wa utekelezaji wa malengo ya kisera ni jukumu la Ofisi ya RaisTAMISEMI ili kuwezesha msukumo chanya katika kufikia malengo ya kitaifa najukumu hili ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ibara ya 146.

“ Kupitia maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa pamoja tumeweza kushirikiana katika kusukuma maendeleo eneo la afya ya msingi na kufanikiwa kusogeza huduma hizi karibu zaidi na Wananchi kwa kuwezesha ujenzi wa Zahanati 1198, Vituo vya Afya 487 na Hospitaliza Halmashauri 99, Tayari huduma zimeanza kutolewa katika vituo mbalimbali nchini ameeleza”, Dkt. Gwajima.

“Haya ni mapinduzi makubwa katika nchi yetu kwani unaposema zahanati kwenye Vijiji na vituo vya afya kwenye Kata tafsiri yake ni kuwa huduma zimesogezwa kwa wananchi hivyo hawatapoteza muda tena kwenda umbali mrefu kufuata huduma hizi bali watapata huduma kwa wakati na kurejea kwenyes hughuli za maendeleo zinazochangia kulinda na kukuza uchumiwa kati”, amesisitizaDkt. Gwajima.

Kwa kuongezeaDkt. Gwajima amesema ukubwa wa upanuzi wa miundombinu unalenga kutimiza maono ya Rais Magufuli ya  kumfikia mtanzania mnyonge asiye na uwezo wa kugharamia safari ndefu za kufuata huduma za afya na huu ni mwanzo kwani kazi bado inaendelea.

Mwisho