Home Siasa TUNDU LISSU ACHUKUA FOMU YA URAIS,ATOA NENO

TUNDU LISSU ACHUKUA FOMU YA URAIS,ATOA NENO

0

Mgombea wa Urais ,Tundu Lissu akikabidhiwa Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha CHADEMA  katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Tundu Lissu wakionyesha  Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha CHADEMA  katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 pamoja na Mgombea Mwenza Salum Mwalimu  mara baada ya kuchukua Fomu hizo katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa  leo jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Tundu Lissu  kupitia Chama Cha CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 akisaini Kitabu mara baada ya kuchukua Fomu hizo za Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles.

Mgombea wa Urais ,Tundu Lissu akionyesha  Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha CHADEMA  katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma

PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG

……………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mgombea Urais wa Chama cha CHADEMA ,Tundu Lissu amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).
Lissu amefika katika Ofisi ya NEC akiwa ameambatana na Mgombea Mwenza Salum Mwalimu na viongozi mbalimbali wa chama hicho na msafara wa wanachama ambao waliishia nje ya geti la ofisi hiyo kutokana na taratibu za Tume kuwataka waingie wachache.
Baada ya kuchukua fomu , Lissu amesema kuwa ni mara yake ya kwanza kufika Dodoma tangu ashambuliwe kwa risasi Septemba 7, 2017 na kuwa atatembea nchi nzima kutafuta wadhamini kwenye mikoa 10 kama alivyoelekezwa na Tume.