Home Makala WATANZANIA NI WAELEWA SANA, 2020 TUNACHAGUA MAENDELEO

WATANZANIA NI WAELEWA SANA, 2020 TUNACHAGUA MAENDELEO

0

*****************************

Na Emmanuel J. Shilatu
Uchaguzi Mkuu 2020 unazidi kukolea na kupamba moto ambapo kila chama, kila mgombea anajinadi kivyake kwa sera zake. Hapa ndipo penyewe.
Kuna chama kinahubiri JPM asichaguliwe tena kwa sababu analeta maendeleo ya vitu pasipo maendeleo ya Watu. Hapa ndipo ulaghai wa si-hasa unapoanzia.
Hivi inawezekana vipi kuwa na maendeleo ya Watu bila ya kuwa na maendeleo ya vitu? Unatofautishaje maendeleo ya vitu na maendeleo ya Watu? Mathalani ukinunua gari hayo yatakuwa maendeleo ya kitu au ya Mtu?
Mwanasiasa huyo huyo anayepinga maendeleo ya vitu ndio huyo huyo amepanda gari toka kwake kuna lami mpaka uwanja wa ndege kupanda Air Tanzania ya kumuwahisha hotelini kufanya mkutano na Waandishi wa habari! Hapo anatengaje maendeleo ya vitu na maendeleo ya Watu? Kama haoni vitu ni maendeleo ya Watu angepanda Punda toka Kijijini kwake akaenda chini ya Miti kufanya mikutano kila mahali!
Ukweli unabakia pale pale hakuna maendeleo ya Watu bila maendeleo ya vitu. Hauwezi ukasema Watu wa nchi yangu wana maendeleo bila ya kuwa na maendeleo ya vitu kama vile miundombinu bora ya barabara, viwanja vya ndege, reli ya kisasa ya SGR, Madaraja kama ya Mfugale na ya Ubungo, Mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme kama ule wa Mto Rufiji unaozalisha megawatts 2115; Bila ya kuwajengea Zahanati, Vituo vya afya, hospitali; Au kuwajengea shule, hostel na vyuo; Ama kuwa na maendeleo ya ndege za kisasa kama ndege 10 zilizonunuliwa na Rais Magufuli kwa kipindi cha miaka 5 tu.
Watanzania ni waelewa sana, tunajua hakuna maendeleo ya Watu bila ya kuwa na maendeleo ya vitu kama vilivyoanza kuletwa na Rais Magufuli.
Kuna chama sera yao kubwa ni “Kazi na Bata” yaani wakifika Ikulu ni mwendo wa “Bata” tu yaani starehe kwa kwenda mbele. Hilo Bata linawahusu Wapiga kura Watanzania wote ama ni wao peke yao?
Kwanza kabisa neno “Bata” tu ni neno la kihuni kama yalivyo maneno mengineyo ya kihuni yasiyo na heshima wala staha. Kutumia neno la kihuni ni kufikiria Watanzania wote ni Wahuni. Haya ni matusi makubwa yasiyokubalika.
Tanzania ni nchi ya kistaarabu na pia Ikulu sio bar, club ama Casino ya kufanyia starehe na anasa. Ni sehemu ya heshima kwa ajili ya kulijenga Taifa kwa kuliletea maendeleo.
Watanzania hatuhitaji mambo ya kihuni, Watanzania tunahitaji maendeleo.