Meneja Ufundi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira manispaa ya Songea Souwasa)Jafari Yahaya aliyen oosha mkono akitoa maelelezo kwa wajumbe wa bodi ya mamlaka hiyo waliotembelea mradi wa maji Myangayanga Halmashauri ya mji Mbinga.
***********************************
Na Mwandishi Wetu,
Mbinga
WIZARA ya Maji imetoa shilingi milioni 200,135,522.40 kujenga tenki kubwa la maji linalojengwa na Mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira manispaa ya Songea(Souwasa) ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wake kuboresha huduma ya maji kwa wananchi wa mji wa Mbinga.
Meneja wa Souwasa Mhandisi Patrick Kibasa alisema, kati ya fedha hizo milioni 120,000,000.00 zimetolewa na wizara ya maji kwa ajili kutekeleza mradi huo ambao utakapoanza kutoa huduma utamaliza kero ya maji kwa wakazi takribani elfu kumi na mbili wa kata tatu ya Matarawe , Bethlehem na Ruhuwiko katika Halmashauri ya mji Mbinga.
Hata hivyo, fedha zilizosalia milioni 80,135,522.40 bado hazijatolewa na zinahitajika sana kumalizia kazi zilizosalia katika ujenzi wa tenki hilo ambalo hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 95 na kwa upande wa malipo yaliyotolewa na asilimia 60.
Alisema, katika mradi huo kazi zilizopangwa kufanyika ni kusafisha eneo,kuchimba msingi,kumwaga zege la msingi wa tenki,kusuka nondo kwa ajili ya msingi na kusuka nondo za ukuta wa tenki.
Kibasa alitaja kazi nyingine kumimina zege la ukuta wa tenki,kumimina zege la ukuta wa paa la tenki,kufunga bomba za kuingiza na kutolea maji, na kujenga uzio na kwa mujibu wake, kazi zilizofanyika katika mradi huo ni kusafisha eneo,kuchimba msingi na kumwaga zege la msingi wa tenki.
Aidha, kazi zilizofanyika ni kusuka nondo kwa ajili ya msingi,kusuka nondo za ukuta,kumimina zege la ukuta,kumimina zege la paa na kupiga plasta katika ukuta wa tenki na mradi umekamilika kwa shughuli za ujenzi(civil works) hivyo kazi zilizosalia zinahitaji fedha ili kukamilisha ujenzi wake.
Alisema, kwa sasa tenki hilo haliwezi kutumika mpaka kazi ya usambazaji na ulazaji mabomba ukamilike katika eneo la Lusaka na Mamlaka imeomba shilingi milioni bilioni 1,271,810,561.00 kwa ajili ya ujenzi wa bomba kuu la kusafirisha maji kutoka Kipunga hadi eneo la Mahela.
Kwa upande wake meneja ufundi wa Souwasa Jafari Yahaya alisema, mamlaka hiyo inatekeleza miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma na miradi hiyo inafadhiliwa moja kwa moja Serikali ya Tanzania.
Alitaja miradi hiyo,ujenzi wa mradi mkubwa wa maji katika mji wa Namtumbo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi ml 863,046,567.70 ulioanza kutekelezwa mwezi Oktoba mwaka jana ambao unatarajia kuhudumia wakazi 10,738 wanaoishi katika vitongoji vya mji huo.
Mradi mwingine unaotekelezwa ni wa vijiji vinne vya Litowa,Litisha,Nakahuga na Peramiho B katika halmashauri ya wilaya Songea kwa gharama ya shilingi bilioni 2,457,267,930.00 ambapo mpaka sasa fedha zilizotolewa shilingi 420,000,000.00.
Meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mji wa Mbinga(Mbiuwasa)ambao ni wasimamizi wa mradi huo Patrick Ndunguru alisema, mradi wa tenki la maji utakapoanza kutoa huduma utasaidia kumaliza kero ya maji kwa wakazi takribani 12,500 kutoka kata tatu za Ruhuwiko,Bethlehem na Matarawe.