Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu akifungua mafunzo ya alama sita mpya za usalama barabarani kwa makundi maalumu kushoto wa kwanza mwenye shati jeupe ni Mratibu wa Mradi wa alama sita mpya maalumu za usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu (NCPDRS) mikoa ya Tanga na Mtwara Christopher Mbelwa akifuatiwa na Mwenyekiti wa (NCPDRS) Jutoram Kabatele kulia ni Katibu Mkuu wa (NCPDRS) Hamisi Cheni.
Mratibu wa Mradi wa alama sita mpya maalumu za usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu (NCPDRS) mikoa ya Tanga na Mtwara Christopher Mbelwa akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa (NCPDRS) Jutoram Kabatele kushoto akisistiza jambo wakati wa mafunzo hayo kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu na Katibu Mkuu wa (NCPDRS) Hamisi Cheni
Mwenyekiti wa RSA mkoa wa Tanga Eddo Mwakimwagile akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Tanga na washiriki kushoto ni Mwenyekiti wa (NCPDRS) Jutoram Kabatele na kulia ni Katibu Mkuu wa NCPDRS Hamisi Cheni
……………………………………………..
KAMATI ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu wenye ulemavu imetoa mafunzo ya alama sita mpya za usalama barabarani katika makundi maalumu mkoani Tanga ambazo zitakuwa mkombozi kwao.
Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa YDCP Jijini Tanga na kufunguliwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa mafunzo hayo na Mratibu wa Mradi wa alama sita mpya maalumu za usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu (NCPDRS) mikoa ya Tanga na Mtwara Christopher Mbelwa alisema msimamizi wa uwepo wa alama sita mpya za makundi maalumu.
Ameeleza kuwa mpango huo wa mradi wa utoaji wa elimu na alama mpya sita umefadhiliwa na Foundation for Civil Society (FCS) tokea mwaka 2010 kwa kuanzia mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar na mwaka huu 2020 wamepata ufadhili kwa mikoaya Tanga na Mtwara.
Mratibu huyo amesema kuwa matarajio ya taasisi yao ni kutoa elimu hiyo nchi nzima lakini kwa kuendesha mradi huo ni gharama kubwa hivyo wanapenda kutoa shukrani kwa Foundation for Civil Society (FCS) huku wakijitahidi kutafuta wafadhili wengine.
“Wafadhili hao utakaotafuta watasaidiana na Foundation for Civil Society kuhakikisha mradi huu unakamilika ifikapo mwaka 2022 lakini pia tunatoa Pongeza zetu kwa utekelezaji wa uwekaji barabarani alama hizi kwani tokea tumeingia mkoa wa Tanga tumeziona”amebainisha.
Pamoja na kutoka elimu kwa madereva walengwa, makundi maalumu na jamii kwa ujumla ili wazitambue alama hizo ambazo ni muhimu kwao kuweza kuzifuata.
ameongeza kuwa usafiri salama katika vyombo vya umma akitolea mfano miundombinu ya mabasi, meli,treni na ndege ili kumfanya mtu mwenye ulemavu wa viungo aweze kupanda na kushuka kwa urahisi.
Aidha amesema pia uwepo wa mafunzo ya udereva kwa walio wenye ulemavu ili waweze kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ambapo hiyo ni utekelezaji wa sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004.
Awali ameweka wazizi wakati akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu alisema kwamba vyombo vya kusimamia sheria visipo simama imara madereva wakorofi wataendelea kusababisha ajali.
“Hivyo ni lazima tuhakikisha tunakuwa makini zaidi lakini niwapongeze askari wa usalama barabarani mkoa wa Tanga wamekuwa wakisimama imara zaidi katika kusimamia ipasavyo sheria za usalama”ameeleza
Hata hivyo alisema kwamba mafunzo hayo ni muhimu kwani yatawapa uelewa jamii hiyo na kuweza kuepukana na ajali ambazo wanaweza kukumbana nazo wanapokuwa wakitumia barabara hizo.
“Lakini nisema RSA ni jicho la tatu la usalama barabarani kwani wamekuwa mstari wa mbelea kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa vitendo visivyosahihi barabarani vinavyofanywa na madereva”Amesema