Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kulia akizungumza jambo na baadhi ya maofisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kumalizika kwa halfa fupi ya ufunguzi wa mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) kwa vijana wapatao 150 kutoka Wilaya hiyo nyuma ni mwonekano wa baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo.(Picha na Victor Masangu) Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia akiwa wameketi meza kuu sambamba na viongozi wengine mbali mbali wa serikali pamoja na maofisa wa JWTZ wakati wa ufunguzi wa sherehe za mafunzo ya jeshi la akiba kwa vijana wa kisarawe kushoto kwake ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilaya ya Kisarawe Meja Mohamed Wawa.(Picha na Victor Masangu) Mwonekano wa Picha ya pamoja kwa viongozi mbali mbali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kisarawe sambamba na maofisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo wa katikaati.(Picha na Victor Masangu) Mshauri wa Jeshi la Akiba kutoka Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani Meja Mohamed Wawa akisoma taarifa kwa mgeni rasmi kuhusiana na mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kuchukua miezi minne .(Picha na Victor Masangu) Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kisarawe wakiwa katika meza kuu wakishuhudia uzinduzi rasmi wa mafunzo hayo ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 150 kutoka Kisarawe.(Picha na Victor Masangu)Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya jeshi la akiba kutoka Wilaya ya Kisarawe wakiwa wamesimama mara baada ya kukamilika kwa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.(Picha na Victor Masangu).
*****************************************
VICTOR MASANGU, KISARAWE
VIJANA ambao wanamaliza mafunzo mbali mbali ya jeshi la akiba wametakiwa kuwa wazalendo na nchi yao kwa kuhakikisha wanalinda na kutunza rasilimali zote za Taifa na kuachana kabisa kushiriki katika makundi ya vijiweni na badala yake wajikite zaidi katika kulinda hali ya amani na utulivu kwa wananchi pamoja na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo .
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya jeshi la akiba amabyo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali amewataka pia kulivalia njuga suala la changamoto ya wanafunzi kupata mimba za utotoni na kupelekea kukatisha masomo yao pamoja na kutofumbia macho vitendo vya ubakaji kwa watoto.
“Mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe napenda kuwaasa vijana wote ambao mmepata fursa ya kushiruki katika mafunzo haya ya jeshi la akiba kwa muda wa miezi minne, kikubwa nataka pindi mtakapokamilisha kozi hii ni lazima kwama muwe wazalendo na nchi yenu na kuhakikisha kwamba mnasimamia na kutunza rasilimali zote za Taifa la Tanzania,”alisema Joketi.
Aidha alisema kwamba ana imani kubwa na vijana hao wataweza kuzingatia mafunzo mbali mbali ambayo watayapata katika kipindi chote hicho na kuwakumbusha mambo muhimu ambayo wanayotakiwa kufayafanya ikiwemo kulinda hali amani na utulivu hasa katika kipindi chote cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.
“Napenda kuwakumbusha kwa sasa ni kipindi cha uchaguzi mkuu wa ngazi mbali mbali ikiwemo udiwani, nafasi za ubunge na Urais kwa hivyo ninawaomba sana kuweni makini katika kipindi hiki kwani mnaweza kurubuniwa na watu mbali mbali kwa hivyo ninawaoba sana kuweni makini ili wilaya yetu ya Kisarawe iwe salama na uchaguzi umalizike bila ya kuwa na tatizo lolote,”alisisitiza.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba vijana wote ambao wanashiriki katika mafunzo hayo ya jesho la akiba ni lazima wahakikishe wanakuwa na kadi za kupigia kura kwani ni haki yao ya msingi ya kumchagua kiongozi yoyote kwa lengo la kushirikiana naye katika kuleta chachu ya maendeleo katika Nyanja mbali mbali.
Awali akisoma risala katika ufunguzi huo Mshauri wa jeshi la akiba katika Wilaya ya Kisarawe Meja Mohamed Wawa alibainisha kwamba vijana ambao wanashiriki katika mafunzo hayo wapo 150 na kwamba watafundishwa mambo mb ali mbali ikiwemo kulinda hali ya amani na ulinzi wa nchi yao huku akidai baadhi yao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa yeti vya kuzaliwa.
Nao baadhi ya vijana ambao washiriki mafunzo hayo akiwemo Helihuruma Lifa na Eliwaza Saimon walisema kwamba mafunzo hayo watayatumia vema na uweledi mkubwa katika kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote waliyopatiwa na Mkuu wa Wikaya ikiwemo kulinda rasirimali za taifa pamoja na kudumisha hali ya ulinzi na usalama kwa wananchi kwa kuzingati hseria na taratibu za nchi.
Mafunzo hayo ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 150 wasichana na wavulana kutoka Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani yatachukua kipindi cha miezi minne ambapo yanatarajiwa kumalizika rasmi Novemba 2 mwaka huu.