********************************
Na Silvia Mchuruza
Kagera
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameiagiza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kufika mkoa wa kagera haraka iwezekanavyo kwa kushirikiana na vyama vikuu vya ushirika kuwalipa wakulima wa kahawa ambao wameuza kahawa zao kwenye vyama vya msingi na imeshachukuliwa na vyama vikuu vya ushirika lakini mpaka sasa wamesubilia muda mrefu bila kulipwa pesa yao.
Bashungwa ametoa maagizo hayo alipokuwa akitembelea na kukagua mabanda kwenye Maonesho ya Wakulima “NaneNane” yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu katika viwanja vya Nyakabindi.
Mpaka sasa TADB imeshatoa shilingi bilioni 27 kati ya bilioni 39.6 zilizotengwa kwa ajiri ya uwekezaji na ununuzi wa kahawa kwa msimu wa wa mwaka 2020. Na vyama vilivyonufaika na mkopo ni huu ni pamoja na KDCU, KCU, Ngara Farmers na WAMACU.
Aidha, Bashungwa ameipongeza TADB kwa kazi wanayoendelea kuifanya kwa kuwawezesha wakulima wa kahawa na na kusisitiza ufualiliaji wa karibu na kujiridhisha kuwa wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati na kwa utaratibu unaotakiwa ili kuepusha malalamiko.
ReplyForward |