Katibu wa Sekretarieti ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Seperatus Fella (kushoto), akizungumza na Washiriki wa Kongamano la Kujadili na Kutathimini Mikakati ya Serikali ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, lililofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Mratibu wa Mipango kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), David Hofmeijer, akizungumza na Washiriki wa Kongamano la Kujadili na Kutathimini Mikakati ya Serikali ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, lililofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mwenyeliti wa Sekretarieti ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu, Adatus Magere. Wapili kushoto ni Katibu wa Sekretaireti hiyo, Separatus Fella, na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Wanawake na Watoto-Zanzibar, Najma Chumu.
Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu, Adatus Magere, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Kongamano la Kujadili na Kutathimini Mikakati ya Serikali ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, lililofanyika jijini Dar es Salaam
Katibu wa Sekretarieti ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Seperatus Fella (kushoto), akizungumza na Washiriki wa Kongamano la Kujadili na Kutathimini Mikakati ya Serikali ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, lililofanyika jijini Dar es Salaam
Mwenyeliti wa Sekretarieti ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu, Adatus Magere (wapili kushoto waliokaa), Katibu wa Sekretaireti hiyo, Separatus Fella (kulia), Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Wanawake na Watoto-Zanzibar, Najma Chumu (wapili kulia), na Mratibu wa Mipango kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), David Hofmeijer (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kujadili na Kutathimini Mikakati ya Serikali ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, lililofanyika jijini Dar es Salaam
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Afrikan Lyon, Rahim Kangezi, akizungumza katika Kongamano la Kujadili na Kutathimini Mikakati ya Serikali ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, lililofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kongamnao hilo lilishirikika wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
********************************************************
Na Mwandishi Wetu, MOHA, Dar es Salaam.
KATIBU wa Sekretarieti ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Seperatus Fella amesema watu 61 wamekuhumiwa kosa la kusafirisha binadamu na kesi 12 zikiendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza katika Kongamano la kujadili Biashara hiyo haramu lililofanyika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Tiffany, jijini Dar ss Salaam leo, Fella amesema takwimu hizo ni za kuanzia mwaka 2016 hadi 2020, ambazo zinaongeza kuwa zaidi ya wahanga 557 wameokolewa baada ya kupata matatizo hayo na wanaendelea na shughuli zao nchini.
“Takwimu za 2016 hadi 2020 zinaonesha kuwa watu waliohukumiwa ni 61, kesi 12 zinaendelea katika Mahakama mbalimbali na wahanga wa biashara haramu ya binadamu hapa nchini ni 557,” Alisema Fella.
Katibu Fella amebainisha kuwa changamoto kubwa ya kuendelea kuwepo kwa biashara haramu ya binadamu ni umasikini katika jamii kwani familia nyingi zinapokea fedha kidogo kwa kudanganywa na kutoa mtoto kwenda kufanya kazi mahali bila kujua kama ni kosa, na pia biashara hiyo ufanywa kwa usiri mkubwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Sekretaireti hiyo, Adatus Magere amesema kuwa usafirishaji haramu wa bianadamu unashika nafasi ya tatu katika makosa makubwa ya kimataifa ikiongozwa na biashara haramu ya silaha na biashara ya dawa za kulevya.
“Watu wanaofanya biashara hii haramu inakuwa ni vigumu sana kuwapata mpaka vyombo vya sheria vinapowagundua, takwimu hazionekani katika uhalisia,” alisema Magere.
Magere aliongeza kuwa, “Watu wengi wanaichanganya tatizo la usafirishaji haramu wa binadamu na wahamiaji haramu kama ambao wamekuwa wakipitishwa hapa nchini kupelekwa Afrika Kusini, matatizo haya ni mawili tofauti, la kwanza ni kusafirishwa kwa hiari yao ‘Uhamiaji haramu’, na biashara haramu ya binadamu kwa anayesafirishwa anakuwa hajui malengo ya msafirishaji,” alisema Magere.
Kongamanbo hilo liliwashirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi na limefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).