Afisa Mwandamizi wa TAKUKURU Makao Makuu Bi Dorothea Mrema akitoa elimu dhidi ya mapambano ya rushwa katika wiki ya Nane Nane,Mkoani Simiyu.
Afisa Mwandamizi wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu Bwana Aquilinus Shiduki akitoa elimu dhidi ya mapambano ya rushwa katika wiki ya Nane Nane,Mkoani Simiyu.
Wananchi wa kata ya Nkololo wakifuatilia mikutano hiyo.
Kikundi cha sanaa cha BASEKI cha mkoani Simiyu kikitoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wananchi wa kata yaLuguru.
…………………………………………..
Wakati wananchi wakijiandaa kufanya uchaguzi mkuu,mwezi Oktoba mwaka huu,TAKUKURU imetumia maonesho ya Nane Nane kuelimisha wananchi dhidi ya vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi kupitia gari ya Matangazo katika Wilaya za Bariadi, Busega na Itilima.Kupitia mpango huo hadi sasa wananchi elfu nane wamefikiwa katika kata za Luguru,Matongo,Sapiwi ,Nkololo,Nyakabindi,Dutwa,Muhango,Bariadi ,Sima ,Somanda na Lamadi.
Uelimishaji huu unaenda sambamba na kikundi cha sanaa cha BASEKI cha Mjini Bariadi.Uelimishaji huu unaendelea hadi tarehe 10,Agosti 2020 maonesho yatakapohitimishwa.