Dodoma kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati, ambaye pia ni
Mkuu ya Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi
Athuman Mukunda akijaribu
kuendesha Trekta kwenye maonesho hayo
leo, aliye pembeni yake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Prof. Elisante Ole Gabriel, walio
chini mwenye miwani ni Katibu Tawala
Mkoa wa Singida Dkt. Anjelina Lutambi na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Injinia
Jackson Masaka wakishuhudia tukio hilo. Picha na John Mapepele
kwenye maonesho ya nanenane kanda ya kati kwenye viwanja vya Nzuguni jijini
Dodoma. Picha na John Mapepele
picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa
mashindano maalum ya Paredi ya mifugo iliyofanyika kwenye maonesho ya
nanenane kanda ya kati kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. Picha na John
Mapepele
Wakuu wa Mikoa ya Singida na Dodoma
kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda
ya Kati,ambaye ni Mkuu ya Wilaya ya
Bahi, Mwanahamisi Athuman Mukunda(mwenye
kilemba) akimuuliza maswali muoneshaji wa kampuni la uzalishaji wa chakula cha
mifugo ya Harsho Group, Juma Ally (mwenye Tisheti ya Njano) Kulia ni Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Anjelina Lutambi. Picha na John Mapepele
Wakuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida wameiomba Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii kuyafanya mashindano
maalum ya Paredi ya Mifugo yanayofanyika kila mwaka kwenye kanda ya kati kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma kuwa Maonesho ya Kimataifa ya utalii wa mifugo ili kuongeza pato la
taifa na kuleta hamasa kwa wananchi kushiriki.
Katika hotuba iliyotolewa kwenye Paredi la Mifugo leo na Mkuu ya Wilaya
ya Bahi Mwanahamisi Athuman Mukunda kwa
niaba ya Wakuu hao wa Mikoa, amesema Tanzania imebarikiwa kuwa nchi ya
pili kwa kuwa na mifugo mingi barani
Afrika hiyo uanzishaji uboreshaji wa Paredi
la mifugo utasaidia kuinua uchumi wa taifa kwa kuongeza kipato kutoka kwa watalii kupitia mifugo.
Ameongeza kuwa jiografia ya Dodoma kuwa katika ya nchi na hali ya hewa nzuri ya majira ya mwezi Agosti
katika eneo la Nzuguni linafanya watalii
wengi kuja kutembelea maonesho hayo.
“Ndugu zangu niwaambie ukweli katika nchi yetu miongoni mwa Wizara mama
ambazo ni nguzo na tegemeo wa maisha ya wananchi wake na ambayo inaweza
kuongeza mapato ya Serikali ni Wizara ya
Mifugo na Uvuvi” alisisitiza Mhe.
Mukunda
Amesema mifugo na uvuvi ni dhahabu inayotembea ambayo kama itatunzwa
kwa kuzingatia ushauri na utaalam
utaongeza tija na kulifanya taifa lisonge mbele
kiuchumi.
Hata hivyo amesema changamoto inayosababisha kutokuwa na mageuzi ya
haraka kwenye Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini ni kukosekana kwa wataalam
kwenye ngazi za chini kwa wananchi
ambapo amesisitiza kuwa kuna umuhimu
Wizara husika kushusha wataalam hadi kwenye ngazi za vijiji badala yahali ilivyo sasa ambapo wataalam wapo kwenye ngazi za juu jambo ambalo
linafanya utalaamu usiwafikie wananchi kama ilivyokusudiwa.
Aidha ameongeza kuwa kuna haja ya Wizara husika kuboresha ushirikiano
katika utekelezaji na utoaji wa
maelekezo ambapo amesema kumekuwa na
ushahidi kuwa sehemu ambazo wizara zimeshirikiana kikamilifu na Halmashauri
husika kumekuwa na matokeo chanya.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa
Singida Dkt. Anjelina Lutambi amepongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kazi
kubwa anayoifanya kwenye Sekta mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na
Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambapo ameelekeza
Halmashauri za Mkoa wa Singida kutenga maeneo kwa ajili ya kulima malisho ya mifugo na ameishukuru Wizara ya Mifugo kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Ikungi kuanzisha shamba darasa bora la malisho ya mifugo ambalo ni la mfano
hapa nchini.
“Ukiona Mheshimiwa, Rais Dkt. John Magufuli anawekeza kwenye miradi kama
ule wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere Rufiji, Reli ya kisasa kutoka Dar es
Salaam hadi Makutupola ya Singida lengo ni kujenga uchumi jumuishi” ameongeza
Dkt. Lutambi
Amesema Mkoa wa Singida umendelea kupiga hatua katika kutekeleza miradi mbalimbali ambapo amesema licha ya
kufanya mapinduzi makubwa kwenye zao la Korosho pia wamesimamia vizuri sekta nyingine kama vile
sekta ya madini ambapo muelekeo wa sekta ya madini ni kuwafanya wananchi
wamiliki raslimali hii kwa kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina amesema Serikali
ya awamu ya Tano imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya mifugo ambapo viwanda vingi vya nyama vimeanzishwa, kuboresha kwa miundombinu ya
mifugo kama majosho na kuimarisha
minada, kuzuia utoroshaji wa
mifugo kwenda nchi jirani na
kuanza kutengeneza chanjo za mifugo ambapo hadi sasa chanjo sita
zimekamilika na nyingine saba
zinatarajia kukamilika katika kipindi
kifupi kijacho na kufanya
chanjo dhidi ya magonjwa 13 za
kipaombele kukamilika.
Aidha, amesema Wizara ya Mifugo
tayari imeshatangaza rasmi tarehe
13/5/2020 bei elekezi za chanjo za
wanyama dhidi ya magonjwa 13 ya kipaombele
kwa mujibu wa Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Na. 17 za Mwaka 2020 kifungu cha 3(2)(g) na Kanuni za Chanjo na
Uchanjaji Na 180 za Mwaka 2020 Kifungu cha 14(b) na (c) ambapo bei ya dukani nay a kuchanjia kwa dozi
haitazidi viwango vilivyoainishwa.