Na mwandishi wetu, Geita
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kupitia idara ya masoko, limeendelea na kampeni yake ya kutoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa migodi na wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka safari hii mkoani Geita.
Migodi iliyotembelewa na kikosi kazi hicho cha TANESCO ni pamoja na Migodi ya Geita
mjini, Wilaya za Nyanghwale na Bukombe, lakini pia mashine za posho mills zilizotembelewa ni za Buseresere Kasamwa, Nyanghwale,Bukombe, Katoro na Geita
mjini.
Kwa mujibu wa Eng Ally Koya kutoka kitengo cha masoko Tanesco makao makuu alisema lengo hasa la kampeni hiyo ni kuwawezesha kufahamu jinsi ya kupunguza gharama ambazo si za lazima kwa kununua vifaa vya kisasa na kuachana na vifaa
vilivyochakaa na vya zamani kwani vinatumia umeme mwingi.
Wamiliki hao walielimishwa kuhusu utaraibu wa kufunga motor za kisasa na kuzifanyia service mara kwa Mara ili motor iendelee kuwa na ufanisi.
“Matumizi bora na sahihi ya umeme ni muhimu kwa usalama kwani umeme ni nzuri kama ukiutumia kwa kuzingatia usalama
lakini pia umeme ni moto mara moja.” Alisema Mhandisi………….
Walipewa pia elimu ya kufunga power factor ili iweze kuwasaidia uendeshaji wa mitambo yaani kVA haitakuwa kubwa.
Aidha wamiliki wa migodi na mashine walishukuru ujio wa wataalamu hao wa TANESCO kwani umewaongezea uelewa na hivyo kuongeza ufanisi katika eneo la matumizi sahihi ya nishati hiyo ya umeme.