Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wadau wa lugha ya Kiswahili (hawapo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam kujadili kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya BAKITA, Dkt. Method Samwel na kulia ni Kaimu mtendaji Mkuu wa BAKITA Bi. Consolata Mushi. Kaimu Mtendaji Mkuu wa baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Consolata Mushi akizungumza na wadau wa lugha ya Kiswahili (hawapo pichani) wakati wa kujadili kanuni za baraza hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya BAKITA, Dkt. Method Samwel. Baadhi ya wadau wa lugha ya Kiswahili wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) ) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam kujadili kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na mdau wa lugha ya Kiswahili Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa kujadili kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Method Samwel (kushoto) akizungumza na wadau wa lugha ya Kiswahili (hawapo pichani) wakati wa kujadili kanuni za baraza hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa BAKITA Bi. Consolata Mushi.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.
***************************
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wadau wa lugha ya Kiswahili kufuata matumizi sahihi ya ithibati ya lugha ya Kiswahili katika matumizi mbalimbali ya lugha hiyo.
Akizungumza na wadau hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam, Waziri Mwakyembe amewahakikishia wadau hao kuwa lugha ya Kiswahili itaendelea kufanya vizuri duniani iwapo itatumika kwa kufuata matumizi sahihi ya lugha hiyo.
“Nawahakikishia lugha ya Kiswahili itaendelea kufanya vizuri duniani kama tutafuata ithibati ya lugha ya Kiswahili kwa matumizi sahihi ya maneno mbalimbali pale tunapoitumia kwa ufasaha,” alisema Waziri Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe amewaagiza wachapishaji wote kuhakikisha wanapata ithibati toka BAKITA kabla ya kuchapisha vitabu vyao na iwapo itabainika hakina ithibati mchapishaji huyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Waziri Mwakyembe amewataka wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kutumia ithibati ya Kiswahili katika kutoa maelekezo ya matumizi ya bidhaa wanazozizalisha ili kumrahisishia mtumiaji wa bidhaa hiyo .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Method Samwel amesema kuwa wafundishaji wa lugha ya Kiswahili wanatakiwa kuwa na vyeti vya utambuzi toka BAKITA kwani jambo hili litasaidia kuondoa vituo visivyo kidhi vigezo.
Mkutano huu wa wadau wa lugha ya Kiswahilinchini una lengola kujadili masuala mbalimbali kuhusu kuboresha kanuni za Baraza la Kiswahili ili kumuweza mtumiaji kutumia Kiswahili kwa ufasaha bila ya ukengeushi.