Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya wanafunzi Jimbo la Jilin Bw.Ahidi Sinene,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati akitoa shukrani kwa Rais Dkt.Magufuli kwa kutuma ndege ya kuwachukua wanafunzi waliokuwa wamekwama nchini China kutoka na ugonjwa wa Corona ,kulia ni Mwanafunzi anayeendelea kusoma nchini China Yazid Iddi na kushoto ni Mwanafunzi Mhitimu Irene Raymond
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WANAFUNZI 252 rai wa Tanzania waliokuwa wamefungiwa Nchini China kutokana na Covid-19 wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe kwa kuwatumia ndege ya kuwarudisha nchini .
Wanafunzi hao wamesema kuwa Rais John Magufuli ana moyo wa upendo katika kuwatumikia wananchi wake bila kubagua .
Aidha wanafunzi hao wakishukuru jijini Dodoma katika nyakati tofauti wamesema Rais Magufuli amewatendea jambo jema kutokana na kutuma ndege ya ATCL Jijini Gwanchue China na kuwarudisha nchini Julai 27, mwaka huu
Wameeleza kuwa kwa gharama ya dola 1,219 sawa na Sh milioni 2.7 badala ya gharama kubwa kama wangetumia ndege ya Ephiopia, Misri au Qatar.
Sinene, mwanafunzi ambaye alikuwa Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wanafunzi katika jimbo la Jilini-China alitoa shukrani kwa Rais Magufuli kutoa ndege ya ATLC bila abiria hadi Gwanchue Julai 26 mwaka huu na kurudi siku moja baadaye na wanafunzi hao waliokuwa wamefungiwa miezi sita nchini humo.
Sinene ameeleza kuwa wanafunzi hao kutoka majimbo mbalimbali nchini humo walikusanyika Guangzhou kwa juhudi za Balozi wa Tanzania nchini China Mberwa Kairuki kufanikisha kuwasafirisha kurudi nchini kutoka uwanja wa Guangzhou.
Balozi Kairuki katika kutimiza majukum yake alisafiri kutoka Beijing hadi Gwanchue umbali wa zaidi kilometa 500 kuhakikisha wanafunzi hao wanasafiri.
Sinene ambaye alikuwa akisoma shahada ya uzamili ya Utawala wa Elimu amelipongeza Shirika la Ndege la Tanzania ATCL kwa huduma nzuri na utendaji bora wa wahudumu pamoja wa kitanzania kwenye Noeing 787 kwani kama isingekuwa wao wangetakiwa kupanda ndege za kutua Misri hadi nchini kwa dola 2,500, Ethiopia au Qatar jambo ambalo gharama zingekuwa mara mbili ya hizo walizotumia kurudi nchini.