Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la Dumila Darajani mkoani Morogoro wakati akielekea mkoani Dodoma. Wafanyabiashara wa Dumila Darajani wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kusimama katika eneo hilo wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyabiashara wa Dumila Darajani mara baada ya kuzungumza nao ambapo amewaahidi kuwajengea vibanda vizuri vya kufanyia biashara zao katika eneo hilo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akila Mhindi wa Kuchoma katika eneo la Dumila Darajani wakati aliposimama kuzungumza na wafanyabiashara hao wadogowadogo akiwa njiani kuelekea Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Mhindi wa Kuchoma kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.
PICHA NA IKULU