Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akiongoza Mkutano wa Lishe wenye lengo la Kutathimini Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa halmashauri katika kipindi cha Nusu Mwaka kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana kilichofanyika Jijini Dodoma.
Afisa Lishe Mkoa wa Dodoma, Heriet Carin alitoa takwimu ambazo zimefanikiwa kuongeza kiwango cha uibuaji wa watoto wenye utapiamlo hadi asilimia 79 kutoka katika kipindi cha Juni mwaka huu kutoka asilimia 11 katika kipindi Desemba 2019 kwenye mkutano wa Kutathimini Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kilichofanyika Jijini Dodoma.
Afisa Lishe Halmashauri ya jiji la Dodoma,Semeni Juma akizungumza kwenye mkutano cha wadau wa Lishe wenye lengo la Kutathimini Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa halmashauri katika kipindi cha Nusu Mwaka kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana kilichofanyika Jijini Dodoma.
Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Bahi Bw.Ally Mvungi akitoa tathimini katika mkutano cha wadau wa Lishe wenye lengo la Kutathimini Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa halmashauri katika kipindi cha Nusu Mwaka kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana kilichofanyika Jijini Dodoma.
Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Chemba akitoa taarifa katika mkutano cha wadau wa Lishe wenye lengo la Kutathimini Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa halmashauri katika kipindi cha Nusu Mwaka kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana kilichofanyika Jijini Dodoma.
Afisa Uchechemuzi kutoka PANITA Lishe Endelevu Bw.Faraja Kabitina akieleza kwenye Mkutano cha wadau wa Lishe wenye lengo la Kutathimini Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa halmashauri katika kipindi cha Nusu Mwaka kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana kilichofanyika Jijini Dodoma.
Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Maria Haule akifafanua zaidi kwenye Mkutano cha wadau wa Lishe wenye lengo la Kutathimini Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa halmashauri katika kipindi cha Nusu Mwaka kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana kilichofanyika Jijini Dodoma.
……………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, zimefanikiwa kuongeza kiwango cha uibuaji wa watoto wenye utapiamlo hadi asilimia 79 kutoka katika kipindi cha Juni mwaka huu kutoka asilimia 11 katika kipindi Desemba 2019.
Hayo yamebainishwa na Jijini Dodoma na Mratibu wa Lishe katika Mkoa wa Dodoma, Herieth Carin wakati wa kikao Cha tathmini ya hafua za lishe katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma.
Ambapo amesema halmashauri nyingi zimetekeleza mkataba wa lishe katika kipindi Cha nusu mwaka Kati ya July hadi Desemba mwaka jana.
“Halmashauri zimeongeza kasi ya uibuaji watoto wenye utapiamlo mkali kwa watoto wa chini ya miaka mitano na kutoa matibabu kwa watoto hao,” amesema Carin.
Pia amesema, halmashauri hizo zilitoa mafunzo ya matibabu ya utapiamlo mkali kwa watoa huduma za afya 223 wakiwemo 155 kutoka Mpwapwa, Kongwa (21), Chamwino (19), Bahi (5), Dodoma Jiji (12), Chemba (2), Kondoa (3) na Kondoa Mji (5).
Aidha amesema halmashauri zilifanya ufuatiliaji wa ukusanyaji wa takwimu kwa kuandaa na kusambaza fomu maalumu za kukusanyia taarifa kwa wahudumu ngazi ya jamii pamoja na vituo vya kutolea huduma.
Amesema, hata hivyo kuna baadhi ya halmashauri zilitoa fedha kidogo tofauti na zilivyotenga kwenye bajeti yake kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe ili kupunguza athari za kilishe kwa watoto hao.
Kati ya halmashauri hizo, Chamwino iliongoza kwa kutenda na kutumia fedha nyingi kwa ajili ya afua hiyo, ilitenga Sh milioni 22.4 na kutumia sh milioni 22.3 sawa na asilimia 99 ya fedha hizo.
“Halmashauri ya Bahi ilitenga Sh milioni 54.5 na ikatumia milioni 44.6 sawa na asilimia 82, wakati Mpwapwa ilitenga sh milioni 72.1 na ikatumia sh milioni 55.3 sawa na asilimia 78.
“Halmashauri ya Kondoa Mji ilitenga sh milioni 32.3 lakini ilitumia sh milioni 19.02 sawa na asilimia 59, wakati Kongwa ilitenga sh milioni 86.8 na kutumia sh milioni 50.02 sawa na asilimia 58 ya bajeti.
“Kondoa ilitenga sh milioni 76.2 lakini ikatumia sh milioni 30.7 sawa na asilimia 40, wakati Jiji la Dodoma lilitenga sh milioni 147.03 lakini lilitumia sh milioni 54.7 sawa na asilimia 37, vile vile Chemba ilitenga sh milioni 53.5 ikatumia milioni 11.5 sawa na asilimia 21.”
Amebainisha kuwa Halmashauri kupitia idara zake mtambuka za lishe kama vile idara ya maendeleo ya jamii, elimu, kilimo na ufugaji ziliendelea kutoa elimu kwa jamii namna bora ya kuinua na kuongeza kipato katika ngazi ya kaya kwa kutumia Tasaf na mifuko ya vijana na wanawake na hivyo kupata fedha za kuinua hali zao za lishe.
Pia kupitia idara hizo yalitolewa mafunzo ya kilimo cha mboga na ufugaji wa wanyama wadogo katika halmashauri za Bahi, Mpwapwa, Kongowa, Chamwino, Dodoma Jiji, Kondoa, Kondoa Mjio na Chemba.
“Mafunzo hayo yalitolewa kwa wahudumu wa afya ngazi za jamii 906 kutoka Bahi, Chamwino, Chemba, Mpwapwa, Kongwa, Kondoa na Kondoa Mji kwa kushirikiana na wadau wa Lishe Endelevu, Lishe Dodoma, Boresha Lishe na World Vision” amesema.
Akihitimisha majadiliano kuhusu tathmini hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge kwanza amewapongeza wakurugenzi ambao walitenga fedha katika bajeti zao na wakatumia kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe kwa asilimia kubwa.
Shekimweri amewataka wakurugenzi ambao walitenga fedha lakini hawakutumia kwa ajili ya afua hiyo, kufanya hivyo kwa lengo la kuendelea kupunguza athari za upatiamlo miongoni mwa watoto wa chini ya miaka mitano