Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi akifatilia mrejesho wa Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya miundombinu ndani ya miaka mitano chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI leo Jijini Dodoma .
……………………………………………………………………..
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw, Godwin Kunambi amesema kuwa wamefanikiwa kutatua migogoro ya Aridhi kwa asilimia 80 na asilimia 20 iliobaki ni migogoro ya kawaida ya mtu na mtu, waliyo dhurumiana hiyo yote ni matokeo chanya ya uwajibikaji wa watendaji wa jiji hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Bw.Kunambi wakati alipofanyiwa mahojiano na mwandishi wetu leo jijini Dodoma .
Bw. Kunambi amesema kuwa wamegawa viwanja 3044 kwa wananchi waliyokuwa wamepisha ujenzi wa miradi mbalimbali ilokuwa ikitekelezwa katika maeneo yao ili nawaokwendelea na maisha yao ya kuleta maendeleo.
Aidha Bw.Kunambi ameongeza kuwa jiji la Dodoma linakuwa kwa kasi kutokana na juhudi za Rais Magufuli kuwa wezesha kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mikubwa yenye adhi ya jiji la kimataifa.
“Miradi hiyo ni Soko kuu la Ndugai, Kituo Kikuu cha Mabasi, Kituo cha Maegesho ya Magari makubwa, Mtandao wa Barabara na sehemu ya kupumzika miradi hiyo ikiwa na thamani ya Bilioni 89”, ameeleza Bw.Kunambi.
Bw.Kunambi ameainisha kuwa soko la Ndugai limetumia kiasi cha Bilioni 14.6, stendi kuu ya mabasi Bilioni 24 sehemu ya kupumzika (Chinangali Creation Center) bilioni 2.9 na mtandao wa Barabara ukitumia bilioni 26.7.
Katika hatua nyingine Bw. Kunambi ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo katika jiji la Dodoma na kutunza miundombinu kwani jiji hilo ni la watanzania wote kutokana na kuwa makao makuu ya Nchi.