Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumzaa na watanzania kuwambia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya miundombinu ndani ya miaka mitano.
Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Josephat Kandege akizungumza na watanzania wakati wa hafla ya kutoa mrejesho wa mafanikio ya sekta ya miundombinu ndani ya miaka mitano.
Katibu Mkuu TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamuhanga akisalimia kabla ya kumkaribisha waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo wakati wa kutoa mrejesho kwa watanzania nini kimefanyika katika sekta ya miundombinu ndani ya miaka mitano.
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI wakifatilia mrejesho wa kilichofanyika katika sekta ya miundombuni ndani ya miaka mitano.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumzaa na watanzania kuwambia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya miundombinu ndani ya miaka mitano.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi wakifatilia kwa umakini uwasilishaji wa mafanikio yaliyofanyikandani ya miaka mitano chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumzaa na watanzania kuwambia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya miundombinu ndani ya miaka mitano.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akipatiwa maelekezo na mtaalamu wa sekta ya miundombin juu ya kilichofanyika ndani ya miaka mitano
…………………………………………………….
Na. Alex Sonna, Dodoma
Serikali imetoa wito kwa watanzania kutunza miundombinu mbali mbali iliowekezwa na serikali nchini ili kuendelea kuwekeza fedha katika maeneo mengine na kuleta maendeleo zaidi katika nchi.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati wa akitoa mrejesho wa mafanikio yaliopatikana katika sekta ya miundombinu ndani ya miaka mitano 2015 – 2020 leo Jijini Dodoma katika wiki ya TAMISEMI.
Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa ni wajibu wa kila mtanzania kulinda miundombinu hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa serikali pale ambapo wanaona kuna watu ambao wanakwenda kinyume na taratib za utumiaji wa miundombinu iliopo katika maeneo yao.
“Wale wanao ng’oa taa za barabarani, alama za barabarani, wanaozidisha kipimo cha ubebaji mizigo kwenye barabara zilizojengwa mijini na vijijini hao wat sio wema kwa nchi yetu kwani wanarudisha maendeleo ya Taifa letu nyuma”,ameeleza Mhe. Jafo.
Mhe. Jafo amesema kuwa watanzania wafahamu kuwa sekta ya miundombinu nchini imesaidia watanzania kuinua uchumi wao na kufanyikisha taifa linafikia uchumi wa kati kwani wananchi sasa wanasafirisha mazao yao bila changamoto kama ilivyo kuwa hapo awali.
“Neema hiyo ni kutokana na maono ya Rais Magufuli aliyetoa kias cha shilingi Tirioni 3.6 kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu mbali mbali ili wananchi kupata huduma za kijamii bila vikwazo hususani mtandao wa barabara za mijini na vijijini”, amebainisha Mhe.Jafo.
Lakini pia Mhe. Jafo amesema kupitia sekta hii zaidi ya vituo vya mabasi 24 vya kisasa vimejengwa katika maeneo mbali mbali nchini kwa lengo la watanzania kupatiwa hduma sahihi kutokana na kodi zao.
Mhe. Jafo ameongeza kuwa sehemu za kupumzika nane nchini zimejengwa kisasa ili pale mwananchi akiwa amechoka kutoka katika majukum yake anapitia pale kupumzika na akili yake kuwa sawa na kuendelea na majukum yake ya utafutaji.
Katika hatu Nyingine Mhe. Jafo ameeleza majukum makubwa na mafanikio ya sekta ya miundombinu chini ya TAMISEMI kuwa ni ujenzi wa machinjio ya kisasa, ofisi mpya za wakuu wa wilaya, nyumba za wakuu wa wilaya na ujenzi wa masoko ya kisasa nchini.
Mhe. Jafo ametoa shkrani za dhati kwa watendaji wake wote kwa ushirikiano waliompatia katika kufanyikisha TAMISEMI inajibu matatizo ya watanzania kwa kuwasogezea huduma za kijamii katika ngazi za msingi na kutatua kero zao kwa wakati ili kusukuma maendeleo kwa ujumla.
Naye Naibu Waziri TAMISEMI, Josephat Kandege amesema kuwa matunda ya mafanikio yote yanayoshuhudiwa na watanzania ni kutokana na ushirikiano mzuri wa watendaji waliokuwa wakionyesha katika kutoa huduma kwa watanzania.
“Mafaniko uletwa na ushirikiano mzuri baina ya watendaji hivyo matokeo yake ni kupata maelengo chanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi waliompa mpa dhamana Rais Magufuli na yeye kuamua kuona tunafaha kuwa wasaidizi wake katika kuwatumikia watanzania”, amesisitiza Mhe.Kandege.