Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri M Kuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki amelitaka Shirika la Mawasiliani Tanzania TTCL, kuongeza nguvu kwa Kampuni yake Tanzu ya T-Pesa ili iweze kwenda na kasi ya ushindani wa Kampuni za kifedha hapa nchini.
Waziri Kairuki alitoa rai hiyo alipotembelea banda la TTCL katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Amesema kwa Sasa Shirika kwa linafanya vizuri ikilinganishwa na awali na kuongeza kuwa ili kuendelea kuliteka soko TTCL hawana budi kuwekeza katika Kampuni ya T-Pesa ili kuwawezesha wananchi na hasa Wakulima, Wavuvi na wafugaji kujiepusha kuporwa pesa zao baada ya mauzo kwakuwa fedha zao zitakuwa salama katika simu zao
Waziri Kairuki alitembelea banda la TTCL akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kwenye Siku ya Ushirika iliyofanyika mkoani Simiyu katika msimu huu wa maonesho ya Nanenane.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ya Maonesho hayo yanayofanyika katika Mkoa wa Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo ni “Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi chagua Viongozi Bora 2020”