Mdau wa filamu nchini, Ahmed Olotu maarufu Mzee Chillo akichangia mada wakati wa uzinduzi rasmi wa kanuni mpya za Bodi ya filamu nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akionesha kanuni mpya za bodi ya filamu kwa waandishi wa habari na wadau wa filamu (hawapo pichani) nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Frown Nyoni na kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Dkt. Kiagho Kilonzo. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wadau wa filamu wakati akizindua kanuni mpya za Bodi ya filamu nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam Baadhi ya wadau wa filamu nchini wakimsikiliza Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa kanuni mpya za Bodi ya filamu nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kiagho Kilonzo (kulia) akizungumza na wadau wa filamu na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa kanuni mpya za bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa Frown Nyoni.
Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini, Profesa Frown Nyoni (kushoto) akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kuzindua rasmi kanuni mpya za bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Dkt. Kiagho Kilonzo.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wadau wa filamu (hawapo pichani) wakati akizindua kanuni mpya za Bodi ya filamu nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Frown Nyoni na kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Dkt. Kiagho Kilonzo.
Picha na WHUSM –Dar es Salaam
*****************************
Na. WHUSM – Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wasani wa filamu nchini kufanya kazi zenye ubora na viwango vya juu ili kuboresha maslahi yao maslahi yao na kushindana na soko la nje .
Akizungumza na wadau wa filamu nchini wakati wa uzinduzi wa kanuni mpya za Bodi ya filamu nchini, Waziri Mwakyembe amewataka wasanii kutumia maboresho ya kanuni hizo kwa kufanya kazi zenye ubora na viwango vya juu katika soko la ushindani.
“Ni wakati sasa kwa wasanii wa filamu nchini kufanya kazi nzuri kwani kanuni hizi zimepunguza tozo na ada mbalimbali kwa kiwango kikubwa lengo likiwa ni kumuwezesha msanii wa filamu nchini kufanya kazi katika mazingira mazuri,” alisema Waziri Dkt. Mwakyembe.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini, Profesa Frown Nyoni amesema kuwa kuanza kutumika kwa kanuni hizi kutapanua wigo kwa wasanii nchini kuongeza kipato kwani kila kazi ya msanii itakuwa ikilipiwa katika vyombo vya habari.
Kwa upande wake msanii mkongwe nchini Ahmed Olotu maarufu kama Mzee Chillo ameiomba serikali kuangalia namna ambavyo wasanii wa filamu nchini wanaweza kupewa vibali kutumia ofisi mbalimbali za serikali.
“Mgeni rasmi naomba kutumia nafasi hii kuiomba serikali kutupa vibali pale tunapohitaji kufanya kazi katika ofisi mbalimbali za serikali kama mahakama na hata mavazi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwa kufuata taratibu zinazotakiwa ili tuweze kuweka uhalisia katika kazi zetu,” alisema Mzee Chillo.
Uzinduzi wa kanuni hizi za Bodi ya filamu utapelekea kupunguza tozo na ada mbalimbali ambazo zilikuwa ni kikwazo kwa wasanii wa filamu hapa nchini kwa kipindi cha muda mrefu, lengo la kuundwa kwa kanuni hizi ni kutoa hamasa kwa wasanii na wadau kufanya kazi zenye ubora.