…………………………………………………………
Na John Walter-Manyara
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amesema kuwa Jeshi hilo halitawafumbia macho watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili kwa watoto watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 4,2020 alisema kuwa vitendo vya ukatili kwa watoto ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamawananchi wanatakiwa kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa polisi pindi wanapobaini watu wenye kufanya vitendo vya ukatili ikiwemo vya ubakaji.
Akizungumzia tukio la kulawitiwa mtoto lililotokea tarehe 29 Julai 2020 majira ya saa tisa alasiri alisema tukio hilo ni la kuhudhunisha ambapo mtoto mdogo (05) mkazi wa mtaa wa Komoto kata ya Bagara wilaya ya Babati aligundulika kuwa amelawitiwa na mtuhumiwa Yona Zacharia (20) mkulima na mkazi wa mtaa huo.
Alisema mbinu aliyotumia mtuhumiwa huyo ni kumvuta mkono mtoto huyo chumbani kwake wakati mtoto huyo akiwa anacheza na watoto wenzake maeneo ya nyumba ya mtuhumiwa na kisha kuanza kumlawiti baada ya kumlaghai kwa kumpa shilingi mia moja (100).
Kwa mujibu wa Kamanda, chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili kwani kijana huyo anaishi na wazazi wake na bado hajaoa na kwamba alikiri kutenda kosa hilo ambapo kwa upekuzi wa awali alikutwa na mafuta ya mgando aina ya Habibi kama kilainishi.
Kamanda Kasabago amesema upelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.