Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza na wanahabari katika katika kikao cha makatibu wakuu wa wizara ya katiba na sheria kutoka nchi za SADC, Maafisa Waandamizi na Wanasheria kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Nchi za SADC bado zinakabiliwa na mlolongo mrefu wa upitishaji wa sheria za pamoja na zile za kimataifa kutokana na kila nchi kuwa na utaratibu wake.
Ameyasema hayo leo Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Prof. Sifuni Mchome katika kikao cha makatibu wakuu wa wizara ya katiba na sheria kutoka nchi za SADC,maafisa waandamizi na wanasheria kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari Prof.Mchome amesema kuwa kupitia kikao hicho wataweza kujadili kasoro zilizopo na kuzifanyia marekebisho ili kurahisisha upitishwaji wa itifaki na sheria mbalimbali ndani ya ukanda wa SADC.
“Zipo baadhi ya itifaki ndani ya umoja huu lakini hazitiliwi mkazo katika ufuatiliaje wake ikiwemo ya uuzaji wa silaha na udhibiti wa silaha ndogo ambazo zinaingia kinyume na sheria ambapo hivi sasa tumeona ni vyema tuweke itifaki ya kudhibiti swala hili kikamilifu”. Amesema Prof.Mchome.
Sambamba na hayo Prof.Mchome amesema SADC inampango wa kushirikiana kwa pamoja katika maswala ya ulinzi na usalama ili kudhibiti uhalifu.