MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahange akizungumza katika Mkutano na Wafanyabiashara pamoja na watendaji wa jiji, Maafisa Afya, Taasisi za Serikali, Viongozi wa masoko na vikundi vya usafi iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chemba ya wafanya Biashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Deus Nyabiri,akizungumza kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe,akizungumza kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Mfanyabiashara Bw.Idd Issa,akizungumza kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Mchumi kutoka Jiji la Dodoma ,Shabani Juma,akizungumza kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Mfanyabiashara kutoka soko la Sabasaba,akizungumza kwenye Mkutano na wafanyabiashara na uongozi wa Mkoa wa Dodoma uliofanyika jijini hapa wenye lengo la kutatua kero zilizopo.
Sehemu ya wafanyabiashara waliopo Dodoma wakifatilia Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahange akizungumza wakati wa Mkutano na Wafanyabiashara pamoja na watendaji wa jiji, Maafisa Afya, Taasisi za Serikali, Viongozi wa masoko na vikundi vya usafi iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………
Na. Alex Sonna, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahange ametoa wiki mbili (siku 14) kwa Jiji la Dodoma kukaa pamoja na kampuni na vikundi vya usafi ili kuweka mkakati mahususi kuhusu uzoaji taka jijini.
Kauli hiyo imetolewa leo katika Mkutano na Wafanyabiashara pamoja na watendaji wa jiji, maafisa afya, taasisi za serikali, viongozi wa masoko na vikundi vya usafi hivi karibuni .
Dkt. Mahenge amesema kuwa baada ya Kusikia malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu kukithiri uchafu katika masoko ya Jiji .
Aidha Dkt. Mahenge amesema kuwa taasisi hizo zinatakiwa kukutana na kuweka azimio namna bora ya kuzoa taka katika jiji hilo ili wafanya biashara kufanya kazi zao katika mazingira safi na salama kwa afya zao na wateja wao.
“Jiji linatakiwa kujadiliana na Kampuni ya Usafi ya Greenwaste, vikundi vya usafi na viongozi wa masoko jijini ili kuweka utaratibu mzuri wa kuzoa taka,ilikuondoa kero ya kujaa taka katika maeneo mbalimbali jijini.”ameelekeza Dkt Mahenge.
Pia Dkt. Mahenge ameelekeza kuwa mzabuni huyo kuangaliwa mkataba wake kama ana uwezo wa kuzoa taka jijini na ikiwezekana aanze kufanya kazi hiyo usiku badala ya mchana kwani kunakuwa na vurugu nyingi.
Dkt. Mahenge amesema kuunda Kamati yake kufuatilia masuala ya usafi unavyofanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji hilo kutokana na kile kinachoonekana kuwa Kampuni ya CgreenWaste imeshindwa kutokana na kuzidiwa na kazi na kukosa vifaa vya kutosha.
Naye Mkurugenzi wa Jiji, Godwin Kunambi ameeleza kuwa kampuni ya GreenWaste inazoa taka katika kata nane tu za Uhuru, Madukani, Majengo, Viwandani, Kilimani, Tambukareli, Makole na Kiwanja cha Ndege na kata hizo zinazalisha tani 38 za taka kwa siku.
Kunambi amesema kuwa katika kudhibiti utupaji taka holela mitaani mzabuni huyo ameweka makasha makubwa 20 na jiji pia limeweka pia makasha 20 kwa ajili ya kuweka makasha kwa ajili kuhifadhi taka kabla ya kuondolewa na kusafirishwa kwenda dampo.
“Katika usafi wa mazingira Jiji la Dodoma tuna vikundi 96 ambavyo kutokana na uwezo kidogo vinatakiwa kukusanya taka na kufikisha kwenye mapima makubwa yaliyopo mjini na kampuni hiyo inatakiwa kufikisha dampo”, amebainisha Kunambi.
Kwa upande wake Afisa Afya Msafirishaji Taka katika Jiji la Dodoma, John Lugendo amesisitiza kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kujua kwamba sheria ndogo ya jiji inataka majani ya migomba yanatakiwa kusafirisha wenyewe hadi dampo isipokuwa taka nyingine ndizo Jiji linatakiwa kuzoa taka hizo.
Huku Kaimu Afisa Afya wa Jiji, Ally Mfinanga amesema kwa sasa halmashayuri ya Jiji inatumia zaidi ya milioni 25 kwa mwezi kwa ajili ya mafuta ya magari kupeleka taka dampo.