***************************************
NA MWANDISHI WETU
IMEELEZWA kuwa, Vifo vitokanavyo na saratani ya mlango wa kizazi vinaongoza na kuongezeka Tanzania japokuwa ni saratani inayoepukika na kutibika.
Katika kufikia malengo hayo, Wamama na Wasichana wametakiwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ilikujua afya zao na kuepuka tatizo hilo.
Katika kutimiza malengo ya kusaidia jamii na kupambana Saratani ya malango wa kizazi, Mwanadada Iman Hatibu na Dkt. Irene Ketegwe kwa pamoja wameamua kutumia siku yao ya kuzaliwa ya Agosti Mosi (1.8.2020) kuwafikia wadada na Wamama 100 iliwapatiwe uchunguzi wa awali zoezi litakaloendeshwa kwenye Hospitali ya Aga Khan, Dar es salaam.
Akielezea zoezi hilo, Bi Iman Hatibu alisema hii inakuwa ni mara ya kwanza na wanatarajia kulifanya kuwa endelevu ilikufikia jamii kubwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
“Katika kusheherekea siku yetu ya kuzaliwa mwaka huu mimi na Dkt. Irene Ketegwe tunakaribisha wadada na wamama katika Hospitali ya Aga Khan kuanzia saa mbili asubuhi hadi mchana.1 Agosti 2020 tutafanya uchunguzi wa awali bure!.”Alisema Bi. Iman Hatibu.
Aidha, amesema zoezi la uchunguzi ni la gharama kubwa na wamama wengi wanashindwa kumudu gharama hivyo kwa kuthamini Mwanamke siku yao hiyo ya kuzaliwa wameiweka kuwa maalum kwa kuendesha zoezi.
Pia Bi. Iman Hatibu amemalizia kwa kueleza kuwa, wameamua kufanya Agosti Mosi kama siku ya kuwakumbuka Bi. Rosemary Marwa ambaye nae alizaliwa siku kama hiyo alifariki kutokana na Saratani ya kizazi huku pia wakimkumbuka Joseph Shawa ambaye kwa upande wake alizaliwa siku hiyo pia alitangulia mbele za haki.