Baadhi ya wahitimu katika Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro ambao sasa ni watendaji katika taasisi mbalimbali hapa nchini baada ya kuhitimu masomo yao maabara baada ya Hayati Mkapa kutoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro wa awamu ya kwanza akichangia wakati wa masomo baada ya Hayati Mkapa kutoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro wa awamu ya kwanza wakiwa darasani baada ya Hayati Mkapa kutoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro, Prof. Hamza Mstaafa Njozi (wapili kulia) akiwa katika kikao na Wanafunzi wa Chuo hicho (hawapo pichani) baada ya Hayati Mkapa kutoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro wakiwa katika mazingira ya chuo baada ya Hayati Mkapa kutoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro wakiwa katika maabara baada ya Hayati Mkapa kutoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
……………………………………….
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Jambo usilolijua ni kama husiku wa giza hivyo basi hatuna budi kutoka gizani kwa kumjua Hayati Benjamini Mkapa walau kwa machache japo katangulia mbele za haki Mwenyezimungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
Kwa kuanzia tufahamu kuwa Jina Mkapa ni jina la ukoo wa wajomba zake. Ukoo wake ni Matwani. Kwa desturi ya Wamakua watoto hufuata ukoo wa wajomba zao. Isingekua hivyo basi angeitwa Benjamin William Matwani.
Hayati Mkapa alianza shule mwaka 1948 akiwa na miaka 10 lakini alikuwa ndiye mwanafunzi mdogo kuliko wote darasani kwa wakati huo.
Alipohotimu elimu ya msingi alijiunga na seminari ya Junior Benedictine (Kigonsera) kwa masomo ya upadri. Lakini baada ya muda mfupi aliomba kurudi Ndanda kuendelea na “middle school”.
Alikataliwa mara mbili na kuambiwa asali ili roho imuongoze kufanya maamuzi na Baadae aliruhusiwa akarudi Ndanda, kisha akamalizia elimu ya sekondari St.Francis College (Pugu sekondari).
Baba yake alikua Katekista na mhudumu wa mapadri, misheni ya Ndanda na alipenda sana mwanae awe Padri au Daktari.
Alijaribu upadri akashindwa, udaktari hakutaka na kugundua kuwa anapenda zaidi kuwa mwandishi wa habari na mwanasiasa hivyo akaamua kuifuata njia aliyoipenda.
Mwalimu Nyerere ni mmoja kati ya waalimu waliomfundisha Pugu sekondari (wakati huo ikiitwa St.Francis college) na baadae Mwalimu Nyerere akamteua kwenye baraza lake la mawaziri mwaka 1977
Hivyo watanzania tunajambo la kujifunza hasa katika nyakati za viongozi wetu hasa kwa hili la Mwalimu na mwanafunzi wake kufanya kazi pamoja.
Aidha Hayati Mkapa amefanya kazi Radio RTD na magazeti ya chama (Uhuru na Mzalendo) kama mwandishi na Mhariri.
Pia Hayati Mkapa amekuwa mwanadiplomasia na kufanya kazi mashirika mbalimbali ya kimataifa, kabla ya kuingia katika siasa.
Hayati Mkapa amekuwa Waziri wa mambo ya nje kwa vipindi viwili tofauti. Mara ya kwanza 1977 hadi 1980 chini ya Rais Nyerere, kisha mwaka 1985 hadi 1990 chini ya Rais Mwinyi.
Munamo mwaka 1966 alioa akiwa kijana wa miaka 28. Alimuoa mtumishi wa wizara ya Habari, binti mrembo aliyekuwa ndio amehitimu masomo yake nchini Uingereza, aitwaye Anna Joseph Shauri Maro na Ndoa yao ilifungwa ukweni (Moshi) na sio kwao Mtwara.
Hayati Mkapa ni Mkatoliki, na mkewe Anna ni Mlutheri, lakini walifunga ndoa bila kuathiri imani zao na Mkapa alibaki kuwa Mkatoliki kwa maisha yake yote huku Mama Anna akiendelea kuwa Mlutheri hata sasa.
Ndoa ilifungwa Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme (Moshi), kisha ikabarikiwa KKKT, Moshi mjini mnamo Mwaka 2016 walifanya Jubilee ya miaka 50 ya ndoa yao.
Hayati Mkapa na mkewe Anna wamejaliwa watoto wawili Stephan na Nicholas. Aliyefuata nyayo za baba yake katika siasa na utumishi wa umma ni Nicholas ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi.
Hayati Mpaka mbali ya kuwa Rais wa Watanzania wote, wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro watamkumbuka sana kwa nafasi yake ya kipekee kwa kuwepo kwa Chuo hicho.
Hayati Mkapa ndiye ambaye aliyatoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.
Pia yeye ndiye aliyekwenda Chuoni hapo katika uzinduzi wa Chuo hicho mwaka 2005.
Aidha yeye ndiye alikuwa Mgeni rasmi wa kwanza katika Mahafali ya kwanza ya kuwatunuku Shahada wanafunzi 165 wa awamu ya kwanza ya Chuo hicho.
Hivyo Hayati Mkapa atakumbukwa sana na atakuwepo daima katika kumbukumbu za Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa mchango Mkubwa alioutoa kwa Chuo hicho na kupanua wigo wa elimu ya masomo ya juu nchini.