MKUU
wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa ibada
maalumu ya maombolezo iliyofanyika wilayani Muheza kwenye viwanja wa
Jitegemee na kuongozwa na Mkuu huyo wa wilaya na wananchi wakiwemo
viongozi wa dini kwa ajili ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu nchini
Benjamini Mkapa
Padre wa Kanisa katoliki wilayani Muheza
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu akizungumza wakati wa
ibada hiyo maalumu ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu
Benjamini Mkapa kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza
Msanii wa mziki wa Dansi nchini Babu Seya akieleza namna Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa alivyowasaidia wasanii
Msaanii wa Mziki wa Bongo Fleva Mwana FA akizungumza
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu akisaini kitabu cha maombolezo kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza
Bendera ikipepea nusu mlingoti
Sehemu ya viongozi wa dini wilayani Muheza ambao wamejitokeza kwenye ibada hiyo
Sehemu ya wananchi wilayani Muheza ambao wamejitokeza kwenye ibada hiyo
WATANZANIA wametakiwa kumuenzi aliyekuwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu
Hayati Benjamini Mkapa kwa yote aliyowaasa katika uhai wake ikiwemo
suala la uwazi na ukweli.
Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya
ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ibada maalumu ya maombolezo
iliyofanyika wilayani Muheza kwenye viwanja wa Jitegemee na kuongozwa na
Mkuu huyo wa wilaya na wananchi wakiwemo viongozi wa dini.
Alisema
wananchi wa wilaya hiyo walikuwa wakimuona hayati Mkapa akipita
wilayani humo akitokea uwanja wa ndege Jijini Tanga kuelekea Lushoto na
kwa sasa hawawezi kumuona tena hivyo waendelee kumuenzi ikiwemo
kumuombea.
“Ndugu zangu wana Muheza tulikuwa tunamuona Hayati
Mkapa akipita hapa kwetu akitokea uwanja wa ndege Tanga na kuelekea
wilayani Lushoto na sasa hatutamuona tena hiyo tuendelee kumuombea
mwenyezi Mungu”Alisema DC
“Lakini Hayati Mkapa aliwapika
aliwapika uji akaweka sukari na bluu bendi na kuwanywesha hivyo
wanamuombea kwa mola aweze kumuweka mahali pema peponi amani “Alisema DC
Mhandisi Mwanasha.
Alisema kwamba msiba huo ni wa watu wote na
Rais Magufuli yupo kwenye wakati mgumu hivyo tuendeleze maombi ambayo
yatakuwa ni faraja kubwa sana kwao hasa katika kipindi hiki kigumu.
Hata
hivyo alisema kwamba wao kama wilaya wanatoa salamu za pole na kumuomba
mola azidi kuwapa faraja katika kipindi hiki kigumu huku akiwapa pole
familia ya hayati Mkapa .
Awali akizungumza wakati wa halfa
hiyo,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu alisema kwamba
mwenyezi Mungu amemchukua Rais Mstaafu Benjamini Mkapa wakati bado
mchango wake ulikuwa ukihitajika kwenye Taifa huku akiwataka watanzania
kuendelea kumombea.
Alisema kwamba watanzania bado walikuwa
wakimuhitaji hayati Mkapa ambaye alikuwa ni mtu wa uwazi kwa kutaka
maendeleo na kuhakikisha anawainua wanyonge na watu wa chini ili waweze
kunufaika.
“Kwa kweli kuondoka kwa Rais Mstaafu Benjamini Mkapa
ni pengo na litakuwa ni ngumu sana kuzibika kwa sababu alikuwa ni mtu wa
uwazi na ukweli ikiwemo kutaka maendeleo”Alisema
Mkuu huyu wa
wilaya alisema Mkapa alikuwa ni kiongozi mpiganaji ambaye hakusita
kujenga hoja na kuitetea hata wakati alipoondoka madarakani bado alikuwa
na msaada.