Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifuta machozi wakati akielezea namna alivyomjua Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati akihutubia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
………………………………………
Na. Majid Abdulkarim, Dar es Salaam
RAIS DK.John Magufuli ameweka wazi kuwa mzee Benjamin Mkapa ameacha alama kubwa katika maisha yake kwamba yeye ndio shujaa wake na mtu muhimu katika historia ya maisha yake kwamba bila yeye asingekuwepo hapo.
Rais Magufuli amebainisha hayo leo mbele ya umma wa waombolezaji walioshiriki kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
“Bila mzee Mkapa nisengekuwa hapa nilipo, mzee Mkapa ni shujaa wangu na mtu muhimu katika historia ya maisha yangu” ameweka ameeleza Dk.Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema Hata alipopatwa na shida au changamoto mbalimbali mzee Mkapa hakumuacha, hakutaka aanguke alimlea kama mtoto wake .
“Hivyo msinishangae ninavyotokwa machozi, hata mzee Kikwete juzi pale nyumbani alishindwa kujizuia alitokwa na machozi”, amesema Rais Magufuli..
Rais Magufuli ameongeza kuwa kuondoka kwake ni pengo kubwa , kwani nilimzoea sana mzee Mkapa.Hata leo hii anapowaona mzee Ali Hassan Mwinyi na mzee Jakaya kikwete wakiwa peke yao anaumia sana.
Walikuwa kama mapacha, nimesikitika kuona wamebaki wawili tu , hii inaumiza sana, mtambuka siku za karibuni mmeona hawa viongozi wa tatu walikuwa kwenye uzinduzi wa kitabu cha mzee Mkapa, walikuwa pamoja kwenye uzinduzi wa TASAF Awamu ya tatu, kwenye jiwe la msingi la Ikulu ya Chamwino walikuwa pamoja, kwenye mkutano Mkutano Mkuu CCM walikuwa pamoja, hakika ilikuwa inapandeza ukiwaona, leo hii wamebaki wakiwa wawili , hatutamuona tena,”ameuznika Rais Magufuli huku akitokwa machozi.
“Nilizungumza naye naye na akaniambia nisiwe na wasiwasi anaendelea vizuri, sikujua kama yale maneno yalikuwa ya kuniaga.Namshukuru Mungu kwa zawadi ya mzee Mkapa, kazi ameikamilisha,”amesema Raais Magufuli.
Hata hivyo amesema kwa maisha ambayo mzee Mkapa ameyaishi hapa duniani na salamu mbalimbali ambazo zimetolewa zikiwemo za kutoka kwa Baba Mtakatifu Francis ni wazi ameishi maisha yake vizuri hapa duniani na ndivyo vitabu vya dini vinavyofundisha.”Tuishi kwa wema duniani na mwisho wa siku tutavishwa taji.
Rais Magufuli amehitimisha kwa kusema kuwa Watanzania wamedhihirisha umoja na mshikamano, hivyo anawashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kumuombea marehemu.
“Navishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kusimamia amani na utulivu, vyombo vya habari, wasanii waliotunga nyimbo mbalimbali kuhusu mzee Mkapa”, ameshukuru Rais Magufuli.