Wananchi Kijiji cha MwanzugiIgungawakipatahudumaya Maji kwenyevioskivilivyojengwakupitiamradiwausafirishajiwamajiZiwa Viktoria kwendaTabora.
Wananchi Kijiji cha Mwanzugi Igunga wakipata huduma ya Maji kwenye vioski vilivyojengwa kupitia mradi wa usafirishaji wa maji Ziwa Viktoria kwenda Tabora.
Tanki la maji linalohudumia mji wa Igunga.
Wadau wa Sekta ya maji wakishuhudia maj iyalivyofika katika nyumba za wananchi mjini Tabora
……………………………………….
Na, Evaristy Masuha.
Kuna msemo wa Kikerewe kwamba ‘Aliyaebhihile ni weatagata.’ Tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili nikwamba alaye vilivyoiva ndiye hupata joto. Msemo wa Kiswahili unao fanana na huu niule usemao, ‘aisifuye mvua imemnyeshea.’
Moja ya kundi kubwa ambalo linasadifu ukweli wa misemo hii ni wananchi wa mikoa yaTabora, Shinyanga, Mwanza naGeita.
Hawa wamenena kwa lugha tofautitofauti. Kubwa zaidi ni kuipongeza serikali kwa kuwezesha maji ya ziwa Victoria kufika katika miji yao na hatimaye kuondoa changamoto yaupungufu wa maji katika miji hiyo.
Taarifa ya Wizara ya Maji kuhusu miji ya Nzega, Tabora, Igunga na Uyui, inaonesha kuwa Februari mwaka huu 2020 miji yote hiyo pamoja na vijiji 92 vilivyokomaeneohayovimefikiwanahudumayamaji, wakati vijiji kumi vikitarajiwa kufikiwa hivi karibuni.
Hili jambo siyo dogo kwasababu maeneo hayo yamekuwa na hali ya ukame na upungufu wa maji ambao umekuwa ukienda sambamba na ukosefu wa huduma ya maji safi na salama ya kutosheleza kwa saa zote, bila mgao.
Hali hiyo imechangia kuathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya wakazi na wananchi wengine. Magonjwa ya kuambukiza hasa yale yanayo tokana na matumizi ya maji yasiyo salama yamekuwa yakitajwa sana katika maeneo haya.
Malalamiko na mrejesho wa wananchi hao umeifikia serikali na kufanyiwa kazi.
Ni jambo lililo wazi kuwa Awamu hii ya tano imesikia kilio cha wananchi katika maeneo haya na hatimaye kuwa fikishia huduma hiyo muhimu ya maji.
Mafanikio ya upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika ni kuashiria safari mpya ya mafanikio katika Nyanja zote za Maisha.
Kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo youtube yenye viunganishi https://www.youtube.com/watch?v=3mbOrDftDwg Pamoja na https://www.youtube.com/watch?v=0wG6iVJiIOk
Wananchi wa miji hii wa mesikika wakipaza sauti zao kuishukuru serikali kwa kusikia kilio chao.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora (mstaafu) Ndugu Aggrey Mwanri ambaye amekuwa akisikika mara nyingi kwa mipango ya kuifanya Tabora kuwa kama jiji la Toronto, kwa bara la Afrika anasema maji yameileta Toronto ya kweli aliyoihubiri kwa muda mrefu.
Anaenda mbali kwa kueleza kwamba changamoto ya magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji machafu ikiwemo homa ya matumbo na magonjwa ya kuhara imepungua sana mkoani Tabora mara baada ya mradi mpya kufikisha maji katika maeneo ambayo haya kuwa na huduma.
Zaidi, pamoja na hilo anawaalika wawekezaji kuelekeza mkoani Tabora kwani changamoto kubwa za mkoa huo ikiwemo huduma ya maji Serikali imezitatua.
“Hakuna mwekezaji anayetamani kwenda kuwekeza katika eneo ambalo lina uhaba wa maji. Toronto ya kweli sasa imefika. Niwaombe Watanzania wote, wakiwemo wakazi wa Mkoa wa Tabora waliokondani na nje ya nchi waje kuwekeza nyumbani”, Mhe. Mwanri anasema.
Bi. Pili Mweda ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga anasema walikuwa na kawaida ya kuchangia matumizi ya maji na mifugo wakati huo wakitegemea maji kutoka bwawa la Mwanzugi.
Naye Edina Philipo Mkazi wa Igunga anasema iliwahi kutokea wakavamiwa na watu ambao walishindwa kuwa tambua wakati wa kienda kuchota maji nyakati za usiku.
“Mimi mwenyewe niliwahi kukimbizwa usiku nikifuata maji. Bahati nzuri nilikimbia nikapiga kelele aliyekuwa akinikimbiza akaniacha. Kwa kweli ujio wa maji haya umepunguza matatizo mengi ya kifamilia huku kwetu”.
Mathias John, Mkaziwa Ziba Kitongoji cha Igumila wilayani Nzega anasema uhaba wa maji ulikuwa umeleta utaratibu mpya wamaisha.
Badala ya utaratibu wa kawaida wa maji kuchotwa na akina mama, kazi hiyo ili kuwa ikifanywa na akina baba kwa kutumia maguta, mikokoteni au baiskeli.
Akiongea mabadiliko baada ya mradi mpya kuanza kazi, Elifuraha Keflasi Mpanda anayeishi Mtaawa Mwayunge Wilayani Igunga ambaye anasema maji ya memfanya aione fursa mpya ya kilimo cha bustani ya Mboga mboga na ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya biashara.
“Nafurahi sasa nimeiona fursa mpya. Nafyatua matofali, nauza, nalima bustani na kuzalisha mboga mboga ambazo zinaniongezea kipato”.
Mbali na wananchi mkoani Tabora uongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira wilayani Igunga ukiongozwa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Rafaeli Melumba anasema kabla ya mradi kuna wakati serikali ilikuwa inalazimika kuingia gharama kubwa kusomba maji kuwapelekea wananchi kwenye maeneo yao.
“Kwa mfano mwezi wa kumi mwaka jana tulilazimika kuingia gharama ya kusomba maji kuwapelekea wananchi kwenye maeneo yao kutokana na ukame ulio sababisha kukauka kwa mabwa yote likiwemo bwawa la Bulenya ambalo wamekuwa wakilitegemea.” Mhandisi Melumba anasema.
Vilio vyote hivi vinaonesha jinsi tatizo la maji lilivyo kuwa kubwa katika maeneo hayo. Shida hiyo ilikuwa imezalisha utamaduni mpya wa maisha, ugumu wamaisha ulikuwa umebadilika kuwa halihalisi ya maisha ya Igunga. Sasa hali imebadilika. Ujio wa maji unafungua fursa nyingi za kiuchumi mkoani Tabora na kupunguza gharama za maisha kwa familia za wananchi.
Mmoja wa wanufaika wa mradi huo Mzee Lumanila Kija wa Kijiji cha Ziba wilayani Nzega anasema gharama za maji zimepungua kutoka kati ya shillingi 500 hadi 1000 kwa ndoo na kwa sasa kuwa shilingi 30 hadi 50 kwa ndoo.
Mzee anasema kama sio umri wake, angekuwa bado ni kijana, angeweza kufanya makubwa kwa sababu alishindwa kufanya mengi wakati wake kutokanana sehemu kubwa ya maisha yake kutumia muda mwingi katika utafutaji wa maji kwa matumizi mbali mbali ya familia.
Maji yamefungua fursa mpya za kibiashara. Adamu John wakijiji cha Ziba anasema ujio wa maji umemfanya aanzebiashara ya kuuza maji ambapo kwasasa anawapelekea wananchi majumbani mwao hasa wale ambao hawana nafasi ya kufika kwenye vioski vilivyojengwa na serikali kwaajili ya kutoa huduma hiyo kwa wananchi wote. Kazihiyoimemuwezeshakununuabaiskelimpyanakuanzaujenziwanyumbayakudumu.
Maji yameleta fursa ya kilimo cha biashara. Sadda Juma mkazi wa Nzega anasema sasa anaweza kulima mbogamboga kwa ajili yac hakula cha familia na ziada anayoipata anafanya biashara.
Agostino Petro Maridadi, Mkazi wa Mwanzugi Igunga anasema sasa nimfanyabiashara watofali. Anafyatua, kuchoma na kuuza.
Hilo limemsaidia kujikwamua kiuchumi na kukidhi mahitaji ya familia na kuwa saidia ndugu zake wengine katika shughuli mbalimbali za kijamii.
Hili ni jambo kubwa la faraja kwa wananchi. Ni jambo ambalo Serikeli yoyote inayojali maslahi ya umma italizingatia.
Heri kwa wana-Igunga, Heri kwaWatanzania. Heri kwaSerikali ya awamu ya Tano. Ndoto ya kumtua mama ndoo imetimia na kazi inaendelea katika maeneo mengine kuwa letea huduma ya maji Watanzania.