………………………………………………….
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini,mkoani Pwani kimeungana na watanzania wote kumkumbuka marehemu Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkàpa na kusema kitaendelea kumkumbuka kwa utawala wake wa UWAZI na UKWELI.
Mwenyekiti wa chama hicho ,Maulid Bundala anaeleza ,pia Mkapa atakumbukwa kwa kupiga vita rushwa ,mchapakazi ,mwenye maono ambae kizazi cha sasa kitakwenda kumkumbuka na kumuenzi nayo.
“Ni mkombozi wa wanyonge kwani alipenda kila mmoja aishi kwa amani bila kuonewa ,kutendewa haki ,na alikuwa mshauri na mwanadiplomasia mzuri ” alisema Bundala .
Nae mkazi wa Mailmoja ,Neema Lucas anaeleza Mkapa ametulea vizuri na ameimarisha amani na upendo kwa Watanzania .
Alikuwa mpenda Uwazi na Ukweli katika utendaji kazi ,maadili kazini ,alipigania kila mmoja afanye kazi ili kujiendesha kimaisha .
Mkazi mwingine Patrick Namahuta, anafafanua kwamba , atamkumbuka Mkapa kwa kuondoa kodi ya kichwa kwani aliweza kupambana na kuondoa kodi ya kichwa na kuomba wananchi waendelee kumuenzi kwa kusoma kitabu cha maisha yake ambacho amekitunga mwenyewe kabla ya umati wake .