Msimamo wa Ligi Kuu Bara
******************************
LIGI Kuu Tanzania Bara leo imefunga pazia lake la mwisho kwa timu 10 kushuka uwanjani kusaka ushindi na baada ya dakika tisini kukamilika imejulikana mbivu na mbichi.
Vita kubwa ilikuwa ni kwenye timu zinazosaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi, kucheza playoff pamoja na zile zitakazoungana na Singida United kushuka daraja.
Baada ya dakika 90 kukamilika pointi zimewahukumu wakali watatu ndani ya ligi ambao maisha yao kwa msimu ujao yatakuwa ni ndani ya Ligi Daraja la Kwanza huku wawili wakisaka nafasi kupitia play off.
Wakali hao watatu wanaungana na Singida United na kufanya jumla ziwe timu nne ambazo zinashuka jumla daraja.
Alliance FC iliyo nafasi ya 17 kwenye msimamo ikiwa na pointi 45, Lipuli FC iliyo nafasi ya 18 na pointi 44, Ndanda iliyo nafasi ya 19 na pointi 41 pamoja na Singida United united iliyo nafasi ya 20 na pointi 18.
Zitakazocheza play off ili kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi ni Mbao FC iliyo nafasi 15 na pointi 45 na Mbeya City iliyo nafasi ya 16 na pointi 45.
Hivyo basi na katika matokeo Lipuli 0-1 Yanga aliyewashusha jumla daraja ni David Molinga dakika ya 38.
Polisi Tanzania 1-2 Simba kwa Polisi Tanzania, Marcel Kaheza dakika ya 30 kwa penalti kwa Simba ni John Bocco dakika ya 2’, 45’+1.
Tanzania Prisons 2-2 Azam kwa Prisons Abdallah Heri 11’ OG, Vedastus Mwihambi 39’ kwa Azam FC, Jumanne Elifadhili Og1’, Never Tigere 59.
Mbao 2-0 Ndanda walioishusha Ndanda ni Jordan John 66, Wazir Junior 18.
Mtibwa 2-1 Ruvu kwa Mtibwa Sugar ni Boban Zilintusa 51’, 65’ Ruvu ni Sadat Mohamed 35.
Alliance 3-2 Namungo kwa Alliance ni Martin Kigi dk 1, Israel Patrick dk 25, Juma Nyangi 65 na kwa Namungo Bigirimana 8’, Frank Mkumbo 61.
KMC 0-3 Mbeya, Rehan Kibingu 68’, Abasalom Chidiebele 87’, Peter Mapunda 90’+2 p.
FT: Coastal 0-1 JKT (Najim Magulu 79’).
FT: Mwadui 2-1 Kagera (Wallace Kiango 13’, 17’ p : Nasoro Kapama 68’).
FT: Singida 0-2 Biashara (Deogratius 20’, David Nartey 27’