Askofu Mkuu wa Kanisa la Kanisa la Evangelastic Assembies of God Tanzania(E.A.G.T), Dkt.Brown Mwakipesile akihubili katika ibada ya Jumapili iliyofanyika kanisani hapo Jijini Dodoma.
………………………………………..
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Kanisa la Evangelastic Assembies of God Tanzania(E.A.G.T), limeungana na Taifa kutoa salam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuondokewa na Mzee Mpaka .
Salam hizo zimetolewa leo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kanisa la Evangelastic Assembies of God Tanzania(E.A.G.T), Dkt.Brown Mwakipesile katika ibada ya Jumapili iliyofanyika kanisani hapo maeneo ya Mlimwa Jijini Dodoma.
Dkt. Mwakipesile amesema kuwa wanaungana na watanzania katika kuomboleza msiba wa taifa na afrika nzima kwani Mzee mkapa alikuwa alama kubwa kwa taifa na mataifa ya Afrika.
Aidha Dkt. Mwakipesile amesema kuwa Mzee Mkapa ataenziwa kwa ukweli na uwazi wa Taifa la Tanzania kwa kuwataka watanzania kufichua mambo yote yasiyo faha katika taifa na kutaka taifa lisonge mbele kwa ukweli na uwazi katika kuleta maendeleo.
“Na kweli Mzee Mkapa alifanya kazi kubwa kwa taifa letu hivyo hatuna budi kuyaenzi yale yote aliofanya kwa taifa ili kwa maslai ya watanzania aliokuwa akiwaongoza”,ameeleza Dkt. Mwakipesile.
Dkt. Mwakipesile ameendelea kusema kuwa taifa litamuenzi Mzee Mkapa kwa jinsi alivyoendesha umoja wa kitaifa, ushirikiano kimataifa, kuunganisha taifa la Tanzania na Mataifa mengine.
“Katika utawala wake taifa lilikwa na madeni mengi lakini alisimamia kwa dhati kwa kuanzisha taasisi na vitengo mbali mbali vya kusimamia ukusanyaji wa kodi na kushiriki kikamilifu kwa kendelea kongea na mataifa mbali mbali ambayo hatimaye yalikubali ktusamehe madeni yetu ili tuweze kupata wakati mzuri wa kujenga taifa letu wenyewe”,amebainisha Dkt. Mwakipesile.
Dkt. Mwakipesile amesema kwa kuendelea kuyaenze mema yote ya Mzee Mkapa hivyo yeye na watanzania wanakila sababu ya kumpa pole Rais Magufuli yeye kama kiongozi Mkuu wa Taifa kwa msiba huu ulotokea hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Dkt. Mwakipesile ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuliombea taifa hasa kipindi hiki cha kelekea Uchaguzi Mkuu uutakaofanyika 28 Oktoba Mwaka huu kufanyika kwa amani, Baraka na mafanikio makubwa ili kuweza kupata viongozi bora wanaofaha kwa kuliongoza taifa.
“Hivyo upatikanaji wa viongozi bora watakao tokana kupitia maombi ya taifa itasaidia sana katika kuongeza chachu ya maendeleo katika utendaji wao kwa kulinda amani na utulivu kipindi watakapo kuwa katika nafasi zao kwa kushirikiana na watanzania katika kujenga nchi” amesisitiza Dkt.Mwakipesile.