Home Uncategorized BUSHAKO AIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI UDIWANI CCM KATA YA MULEBA MJINI

BUSHAKO AIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI UDIWANI CCM KATA YA MULEBA MJINI

0
Muhaji Bushako mshindi wa kura za maoni mgombea Udiwani Kta ya Muleba Mjini akijinadi kabla ya kupigiwa kura .
…………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim, Muleba
Wajumbe wa CCM wa Kata ya Muleba Mjini wamefanya maamzi  ya kumchagua Muhaji Bushako kwa kumpigia kura nyingi zilizomfanya aibuke kidedea katika kura za maoni Kata ya Muleba Mjini ngazi ya Udiwani.
Aidha Bushako amesema ndoto yake  nikuona Kata ya Muleba mjini  inatoka ilipo na kuwa mji kamili, ili wajasiliamali wafanye Biashara kwa Uhuru na popote wajisikiapo.
“Hivyo na Kata jirani watakuja kufanya Biashara na kuwekeza kwenye Kata yetu bila woga, na kuondokana na mfumo duni kama ilivyo sasa”,ameeleza Bushako.