Home Biashara Kituo cha Mawasiliano ya  Wateja cha TBL Plc  Chafanikisha Ukuaji wa Biashara za Kampuni

Kituo cha Mawasiliano ya  Wateja cha TBL Plc  Chafanikisha Ukuaji wa Biashara za Kampuni

0

Meneja wa Kituo cha mawasiliano ya  wateja cha TBL plc ,Lello Mmassy akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kituo hicho katika mwaka mmoja  uliofanyika katika ofisi za kituo hicho zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam

Meneja wa Kituo hicho  ,Lello Mmassy (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Plc, Doreen Tumurebire wakikata keki wakati wa hafla ya kuadhimisha mafanikio ya mwaka 1

Wafanyakazi wa kituo hicho  wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuadhimisha mwaka 1 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

…………………………………………………………………………………………….

Kituo cha mawasiliano ya  wateja (CIC) cha kampuni ya bia ya TBL Plc, kilichopo jijini Dar es Salaam, ambacho kilianzishwa mwaka jana kimetoa mchango mkubwa kwa ukuaji wa biashara ya kampuni na ongezeko la mauzo ya bidhaa zake kwa wateja pia kimekubwa mstari wa mbele kufanya ubunifu wa kupanua masoko sambamba na kusikiliza maoni na changamoto za wateja na kuzifanyia kazi.

Akiongea wakati wa kuadhimisha mwaka 1 tangu kianze kutoa huduma, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Plc, Philip Redman alisema “Najivunia kuona mpango huu ukiwa katika majaribio umepata mafanikio makubwa na kuwa injini ya  biashara yetu. Mwaka uliopita tumefanikiwa kubadilisha huduma zetu za biashara kwa wateja wetu, asilimia 40% ya mauzo  kwa wateja wetu wadogo wanahudumiwa na kituo hiki.’’

Redman, aliongeza kusema kuwa wateja wa kampuni wamenufaika kwa kupata huduma kirahisi na wanaweza kununua bidhaa kwa bei nafuu na kuzifikisha katika maeneo yao ya biashara bila kutumia gharama kubwa. Aliongeza kusema kuwa mpango wa kampuni ni kuongeza idadi ya watumiaji huduma za kituo hicho hadi ifikapo mwaka 2021 sambamba na kuendelea kujibu maswali ya wateja na kupokea maoni yao kwa ajili ya kukuza biashara zaidi na sambamba na kutoa huduma bora kwa wateja.

Kupitia mtandao wake mkubwa wa biashara,TBL imekuwa moja ya kampuni inayoendeshwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za biashara nchini Tanzania na mchango wake umekuwa ukitambuliwa na wadau wake mbalimbali kwa uzalishaji wa bidhaa zake kwa kutumia malighafi za ndani kuzalisha bia bora ambazo zimekuwa zikishinda tuzo za kimataifa za ubora sambamba na kuwa chapa zinazopendwa kutumiwa na wengi nchini.

TBL Plc, ni kampuni inayoongoza kwa kutengeneza bia nchini na pia inaongoza kwa uwekezaji katika sekta ya viwanda sambamba na  kuwekeza kwenye  matumizi ya mifumo ya kimataifa ya uzalishaji,kwa wafanyakazi wake na pia inaendelea kuwezesha mnyororo wa wadau wake inaoshirikiana nao kibiashara wanaoiuzia malighafi na mahitaji mbalimbali ya kufanikisha uzalishaji.