************************************
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinawataarifu wahitimu, wadau wa Chuo na umma kwa ujumla kuwa, kufuatia kifo cha Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mahafali ya Hamsini (50), Duru ya Kwanza, yaliyokuwa yafanyike siku ya leo Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City kuanzia saa sita na nusu mchana yameahirishwa mpaka itakapotangazwa tena.
Tunasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, familia ya Mheshimiwa Mkapa na Watanzania kwa ujumla kwa msiba huu mkubwa.