Home Mchanganyiko AJALI YA GARI KUGONGA MAGARI MANNE NA PIKIPIKI YA MATAIRI MATATU NA...

AJALI YA GARI KUGONGA MAGARI MANNE NA PIKIPIKI YA MATAIRI MATATU NA KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.

0

*************************

Mnamo tarehe 21.07.2020 majira ya saa 10:30 Asubuhi huko katika eneo la Mlima Iwambi lililopo katika barabara ya Mbeya – Tunduma Gari lori mali ya Kampuni ya “VESAGE TRADING COMPANY” ya Jijini Dar es Salaam lenye namba za usajili T.952 DJZ likiwa na Tela namba T.277 BNN aina ya Howo likiendeshwa na Dereva aitwaye STEPHEN MATHIAS LUCHAGULA likiwa linashusha mlima likitokea Dar es Salaam kuelekea nchini Zambia likiwa limebeba shehena ya mbolea liligonga Gari DFPA 0464 aina ya Toyota Land Cruiser likiendeshwa na ROBERT PAUL MOLLEL [36] kisha kugonga Gari namba KCX-070A/ZG 2136, Gari namba KBZ 273V/ZF 7136 na Gari namba T.758 CRU aina ya Toyota Vista na kisha kugonga Bajaji namba MC.671 CMX aina ya TVS na kusababisha kifo kwa abiria mmoja mwanamke aliyekuwa kwenye Bajaji ambaye bado hajafahamika jina lake.

Katika ajali hiyo watu watatu wote wanaume wamejeruhiwa ambao ni:-

  1. ROBERT PAUL MOLLEL [36] Dereva wa Gari namba DFPA 0464 aina ya Toyota Land Cruiser
  2. BARAKA MWANSASU [31] Mtunza Data Walter Reed na Mkazi wa Isanga
  3. MUHIDIN HUSEIN NGALAWA [35] Mfanyakazi wa OZY Mining (T) LTD na Mkazi wa Mwanjelwa.

Majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali Teule Ifisi iliyopo katika Mji Mdogo wa Mbalizi. Chanzo cha ajali ni kufeli breki kwa Lori la mizigo. Msako wa kumtafuta Dereva wa Lori unaendelea. 

WITO:

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi SEBASTIAN MBUTA anatoa wito kwa madereva kutii sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata utaratibu uliowekwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya wa kuruhusu magari ya abiria na yale ya mizigo kupita eneo la mlima kwa awamu tofauti ili kuepuka ajali na madhara makubwa yasitoke pindi ajali inapotokea.