Philemon Mollel maarufu Kama Monaban akiomba kura (Happy Lazaro)
Mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini ,Philemon Mollel akizungumza wakati akiomba kura katika mkutano mkuu maalumu wa wajumbe wa CCM wilaya ya Arusha mjini .(Happy Lazaro)
Mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini , Richard Paul akiomba kura kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya wilaya ya kuwachagua wabunge (Happy Lazaro)
******************************
Happy Lazaro,Arusha.
Mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Richard Paul maarufu Marcas ameomba Ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini kutokana na utendaji kazi alioufanya katika jamii.
Alisema kuwa, alishawahi kufanya mambo mbalimbali ikiwemo uanzilishi wa kukusanya mapato ya maegesho ya magari (parking )Mkoa wa Arusha mbali na kazi hiyo pia kazi ingine aliyoifanya ni pamoja na kushauri Twiga benki kuwa benki ya posta Mara baada ya kuona benki hiyo kuwa na matawi manne na kukusanya Madeni na baadaye kuwa moja ya benki kubwa nchini .
Pia alisema kuwa yet ni Mkusanyaji wa madeni sugu mamlaka ya usimamizi wa bandari zote Tanzania pamoja na madai ya madeni sugu ya wanafunzi wa chuo cha bandari .
Alisema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Arusha atasaidia wakina mama wanao panga bidhaa barabarani eneo la francekona wanapata maeneo ya kufanyia biashara zao mahali salama zaidi .
Amewaomba wajumbe kumpa ridhaa kwani jimbo la Arusha linahitaji mtu mwenye maono kama ya kwake ili aweze kusaidiana na Mh John Pombe Magufuli kuendeleza Tanzania ya uchumi wa kati.
Naye mgombea ubunge Jimbo la Arusha mjini,Philemon Mollel (Monaban)alisema kuwa ,atasukuma maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Arusha huku akihakikisha wanaondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Mollel alisema kuwa,anatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo ambapo atahakikisha anashughulikia swala zima la ajira kwa vijana kutokana na uzoefu aliopo nao wa kujenga viwanda Kila kata ambavyo vitakuwa vikitoa ajira pindi watakapompa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho.
Akiongea katika mkutano mkuu maalumu wa kupiga kura za maoni ya kumtafuta mbunge wa jimbo hilo,Monaban alisema kuwa,endapo akipewa ridhaa atahakikisha anabadilisha jimbo kwani jimbo hilo linahitaji mwakilishi mwenye uchu wa maendeleo atakayeleta mabadiliko katika Jimbo hili.
Alisema kuwa,atahakikisha anawezesha wanawake,vijana ,na wazee kupata mikopo ya riba nafuu katika mabenki mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Alinukuu kitabu cha methali 29 mstari 2 inayosema mwenye haki anapotawala watu wanafurahi, lakini mtu muovu atapotawala watu wanateswa ,wanaumia ,hivyo endapo atapata ridhaa atasukuma maendeleo na tumbo.