Muonekano wa jengo jipya la kumpumzikia abiria wanaotumia kivuko cha MV. ILEMELA wakati wakisubiri kivuko, jengo hilo limejengwa upande wa Kayenze wilayani Ilemela mkoani Mwanza na tayari limeanza kutumika.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (wa pili) kushoto akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Mji Anderson Msumba kulia pamoja na meneja wa TEMESA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Margareth Mapela katikati wakati wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya mji huo ambapo TEMESA Kahama imefanya usanifu wa mifumo ya umeme na inasimika umeme katika majengo hayo. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kushoto akiikagua ijnini ya kivuko cha MV. Misungwi ambayo ilikuwa ikifanyiwa matengenezo kinga katika karakana ya kivuko eneo la Kigongo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza mwishoni mwa wiki.
Abiria wakisubiria mabasi yatoke kwenye kivuko ili waweze kupanda kuendelea na safari mara baada ya kushuka kutoka kwenya kivuko cha MV. Mwanza wakitokea upande wa Busisi wilayani Sengerema. Kivuko cha MV. Mwanza kinatoa huduma kati ya Kigongo wilayani Misungwi na Busisi wilayani Sengerema.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto na meneja wa TEMESA Mkoa wa Singida Mhandisi Awadhi Suluo Wakikagua muendelezo wa ukarabati na ujenzi wa majengo mapya ya karakana ya mkoa wa Singida wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo mwishoni mwa wiki hii.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWEN0 (TEMESA)