**********************************
July 20
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
Baada ya kumalizika kwa hatua ya kurejesha fomu kwa wabunge ndani ya ccm ,imeingia hatua ya kura za maoni za ndani ya chama ,ambapo kwa Jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amepata kura 369,akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM Pwani Ramadhani Maneno kura 273 na watatu ni diwani anaemaliza muda wake kata ya Talawanda Saidi Zikatimu aliyepata kura 223.
Na jimbo la Kibaha Vijijini mshindi ni Hamoud Jumaa aliyeibuka na kura 332,Michael Mwakamo 33 na Hussein Chuma 31 wapiga kura 486 iliyoharibika moja.
Matokeo ya Kura za maoni jimbo la Mkuranga ,Idadi ya wapiga kura 1,218
Kura zilizo haribika 4 na halali 1214.
Wagombea ni 15 (1)Abdallah Ulega 1138
(2) Ramadhani Mlao 50
(3)Ally Jumanne Mawe 7
4)Mwasiti Omari 5
5)Ibrahim zambi 3
6)Omari kambangwa 3
7)Ramadhani Pepo 3
8)Dismas Bengese 2
9)Curtius Mwesa 1
10Saidi manzerele 1
11)Nuruel Kavishe 1
12 Jafari Ndande 0
13Dominick salamba 0
14Bruno ng’ing’o. 0
15Eng SALUM ALLY 0
Kura za maoni Jimbo la Kisarawe
Kura zilizopigwa -601
Zilizoharibika – 1
Selemani Jafo -588
Ally Goha -2
Salum Chaurembo -2
Zainab Adam -2
Dr Zemba Mumbi-2
Mohamed Masenga-1
Hassan Bangusiro-1
Fransisco Gorsbert -1
Jimbo la Rufiji ,Mohammed Mchengerwa 273 na Dk.Seif Rashidi120 walikuwa 33 ,Athuman Likeyekeye kura 62 wa tatu.