MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi, wanasiasa na vyombo vya ulinzi na usalama kutimiza wajibu wao tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu kulingana na sheria, kanuni na taratibu kwa kutojiingiza kwenye uhalifu.
IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Maofisa Wakuu Waandamizi Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi, kikao ambacho kimelenga kufanya tathimini ya hali ya uhalifu nchini na kuzungumzia suala la uchaguzi mkuu na kuweka mikakati ya kuhakikisha unakuwa wa amani na utulivu.