MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi akiwahutubia Wanachama wa CCM na Wananchi Pemba katikia uwanja wa Kibirinzi chakechake wakati wa mkutano wake wa kutambulishwa kwa Wananchi uliofanyika leo katika uwanja huo.(Picha na Ikulu) WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi Kisiwani Pemba wakifuatilia hutuba ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiwahutubia katika kiwanja cha Kibirinzi Chakechake Pemba wakati wa mkutano wake wa kutambulishwa uliofanyika leo.(Picha na Ikulu) WALIOKUWA Wabunge wa CUF na sasa wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi wwakimsikiliza Mgombea wa Urais wa CCM katika mkutano wa kutambulishwa kwa Wananchi kisiwani Pemba uliofanyika katika Uwanja wa Watoto Kibirinzi Chakechake Pemba leo.(Picha na Ikulu)MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi waliofika katika vuwanja wa Kibirinzi Chakechake Pemba wakati wa mkutano wa mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi , alipowasili Uwanja wa Ndege Chakechake Pemba kuhudhuria mkutano mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi leo,19-7-2020, (Picha na Ikulu) MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akivishwa shada la maua na kijana wa Chupukizi Zakia Makame na kushoto Mke wa Mgombea Mama Maryam Mwinyi, walipowasili Uwanja wa Ndege Chakechake Pemba leo 19-7-2020, kwa ajili ya kutambulishwa baada ya kuteuliwa kugombea nafasi hiyo kwa Tiketi ya CCM.(Picha na Ikulu) WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi Kisiwani Pemba wakiwa katika barabara ya Chakechake Pemba wakisubiri kumpokea Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi, mapokezi hayo yamefanyika leo 19-7-2020 na kufanyika mkutano wa kumpambulisha katika Uwanja wa Kibirinzi Chakechake Pemba.(Picha na Ikulu) MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali alipowasili Uwanja wa Ndege Chakechake Pemba leo 19-7-2020,(Picha na Ikulu)
*********************************
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezimungu, mwingi wa rehma kwa kutuwezesha kukutana hapa hii leo. Kuwashukuru wananchi wa Pemba kwa mapokezi
makubwa sana. Napata faraja kazi yetu sasa itakamilika mapema sana.
Nashukuru chama kwa kumaliza uteuzi wake kwa kwa haki, na sasa sote tumekua wamoja, hakuna timu Mwinyi wala timu Mbarawa, na lengo letu sasa ni moja kushika dola.
Kabla ya yote tuwaombee wale waliopata maafa Mwenyezi Mungu awarehemu, na wengine waliopata ajali ya kuezuliwa mapaa nyumba zao Mungu awafariji.
Sitosema mengi. Muwe na hakika nitaenzi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964. Nitadumisha Muungano wetu ni wa aina yake, na unatiliwa mfano duniani kote.
Kuna suala kubwa, nalo ni suala la amani na ndio maana tunapata maendeleo. Nchi nyingi za jirani zetu hakuna amani. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuongoza nchi kwa amani.
Jukumu langu ni kuhakikisha amani inadumu. Lazima tudumishe umoja wetu. Kusiwe na Upemba na Uunguja, kusiwe na ukusini na Ukaskazini.
Sote ni Wazanzibari. Suala la ajira tutalishughulikia hasa kwa vijana. Niwapongeze hasa Rais Dkt. Shein na viongozi wote wa serikali na chama.
Nihakikishe alopoachia yeye nitaendeleza. Nitaendeleza miundombinu, huduma za jamii, ustawi wa watu, maendeleo ya jamii, afya, elimu, na yote yanayogusa watu. Nitahakikisha Mzazibari anakua na maisha bora.
Ukitaka kuyafanya hayo, lazima uwajibike. Huwezi kuwa na program kukawa na wala rushwa, wabadhirifu, Wazembe. Sitokua na huruma kwa wenye tabia hizo. Serikali itafanya kazi kwa maslahi ya Wazanzibari
wote.
Wapo wanaosema Mwinyi ni mpole. Mimi Nasema wataniewa.
Nasema haya kwa sababu pengine hamjanisikia nikiongea sana kwenye vyombo vya habari. Sababu kubwa ni kwamba Wizara ya Ulinzi huko mambo yetu ni ya siri hatufanyi hadharani. Siwezi kusema ila kwa wale
wabadhirifu,wala rushwa, wazembe, wasiowajibika, hao watawajibika.
Nitasimamia maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya za Kimataifa.
Nikwambieni nimeamua nigombee na ili nitakaposhinda dhamira yangu ni moja kuwatumikia Wazanzibari wote.
Tukishika dola, tutakuja na miradi ya kusaidia Wazanzibari ikiwemo ajira kwa wote bila ubaguzi.
Panapo dhamira njema Mwenyezi Mungu atatupa neema.
Mwaka huu, tunataka tupate ushindi wa kishindo usiwe mwembemba tukapata malalamiko. Na niliyoyaona Unguja na hapa Pemba kwa sasa sina shaka ushindi ni mkubwa. Sina shaka ushindi utakua ni mkubwa.
Nasema tena kwamba ‘Yajayo yanafurahisha.’ Ni ahadi naichukua mbele ya Mungu na mbele yenu. Nitahakikisha nawahudumia wananchi.
Sasa na wakati huu nina hakika tunafanya mambo mazuri kwa maisha yetu yawe mazuri . Kazi iliyobakia ni kwenda kushika dola na si vyenginevyo. Kwa sasa lililobakia ni umoja mshikamano na ushirikiano ndani ya CCM.
Katika risala ya mikoa miwili ya Pemba ya Kusini na Kaskazini salamu nimezipokea na kuondoka Pemba nikiwa na faraja kubwa hivyo hayo yanaonekana ni mapenzi ya dhati ninaahidi kuitumikia Zanzibar kwa moyo wangu wote. Ihsani hulipwa kwa Ihsani .
Maneno yanayosemwa na wagombea kama wametumwa na Hussein , nataka kuwaambia hapa leo, sijamtuma mtu, kila mtu apambane na hali yake, maana wengine wanasema eti wachaguliwe ili nitakapounda Baraza la
Mawaziri, niwateuwe, nawaambia sijamtuma mtu.
Nataka kurudia maneno aliyosema Kama Makamu Mwenyekitu wetu Rais Dkt Shein kuwa tutumie uchaguzi huu ndani ya Chama kupata wagombea bora.
Baada ya kusema hayo sasa naomba nimalizie kwa kuwashukuru wana CCM na wananchi wote waliojitokeza katika mapokezi yetu na hapa uwanjani.
Zanzibar ni njema atakae aje