MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akitoa maelezo kwa wasimamizi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu tawala wa Wilaya ya Chamwino alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya mkoa wa huo.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa nyumba ya katibu tawala wa wilaya ya Chamwino iliyopo mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akizungumza na Mkandarasi kutoka SUMA JKT anayesimamia ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru iliyopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Muonekano wa jengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa na SUMA JKT iliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akisisitiza kwa Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambapo ametoa wiki mbili kwa SUMA JKT wawe wamekamilisha ujenzi huo.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma huku akitoa wiki mbili kwa SUMA JKT wanaosimamia ujenzi huo wawe wamekalisha.
Muonekana wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma inayojengwa na SUMA JKT.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayesimamia ukarabati wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo ametoa wiki mbili ukarabati huo uwe umekabirika.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akikagua ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma huku akitoa wiki mbili uwe umekamilika.
Mafundi wakiendelea na ukarabati wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo ametoa wiki mbili kwa Mkndarasi kutoka wizara ya ujenzi awe amekamilisha ujenzi huo.
…………………………………………………………………
Na. Alex Sonna, Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge ametoa siku 14 kwa mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya ya Dodoma pamoja na ukarabati wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuwa uwe umekamilika ili viongozi waweze kuhamia humo na kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dodoma akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo iliyo tolewa fedha na hivyo inatakiwa iwe imekamilika kwa wakati.
Aidha Dkt. Mahenge amesema kuwa mkandarasi huyo hataongezewa muda hivyo ni jukumu lake sasa kuhakikisha anaongeza nguvu kazi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.
“kwani katika mradi huu ili kuongeza sipidi inahitajika kuongeza nguvu kazi ya watu ili kukamilisha mradi huu wala sio hoja ya kuongezewa muda’,ameeleza Dkt.Mahenge.
Dkt. Amesema kuwa katika hospitali ya Uhuru changamoto ni muda hivyo ametoa wito kwa Mkandarasi SUMA JKT ifikapo 23 Agosti,2020 kukamilisha na kukabidhi mradi huo kwani uhitaji wa huduma za afya mkoani Dodoma ni mwingi hivyo unahitajika haraka sana kukamilika ili kuanza kufanya kazi.
Katika ziara hiyo Dkt.Mahenge amekagua ujenzi wa nyuma ya Katibu tawala wa wilaya Chamwino ,nyumba ya mkuu wa wilaya Dodoma, ukarabati wa nyumba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Uhuru.