Home Mchanganyiko WILAYA YA KONGWA YA FANYA UBUNIFU KATIKA UTUMIAJI WA CHF ILIYOBORESHWA

WILAYA YA KONGWA YA FANYA UBUNIFU KATIKA UTUMIAJI WA CHF ILIYOBORESHWA

0

……………………………………………..

Na. Alex Sonna, Dodoma

Halimashauri ya Kongwa Mkoani Dodoma imeweka mikakati  Madhubuti ya kuhamasisha wananchi wanahudumiwa na kupata matibabu kwa gharama nafuu kwa kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ya CHF iliyoboreshwa ili kutimiza  adhima ya serikali ya Awamu ya Tano.

Kauli hiyo imebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Dkt. Omary Nkulo alipokuwa akizungumza na waandishi wa hapabri.

Aidha Dkt. Nkulo amesema kuwa  Halmashauri ya wilaya ya Kongwa ni moja ya Halmashauri iliyokuwa ikifanya vizuri sana kwenye Bima ya CHF kutokana na mikakati ya uhamasishaji  waliojiwekea lakini pia ameahidi kama Halmashauri kuendelea kufanya uhamasishaji ili watu wengi zaidi wajiunge na CHF iliyoboreshwa.

“Kwa Kongwa tumejiwekea utaratibu madhubuti wa Uhamasishaji na Timu yangu ya uhamasishaji chini ya Bwana Amos,kwa kweli inafanya kazi nzuri sana,sasa hivi tunakwenda kuhamasisha kwenye nyumba za Ibada,na muitikio ni mkubwa sana,watu wamekuwa wakiuliza maswali na kujiunga na Bima hii,niwaambie tu wananchi wa Kongwa, Serikali yao inawajali sana na ndio maana inataka kuwahudumia kwa gharama nafuu hivyo wajitahidi kuwa na Bima ya CHF”ameeleza Dkt. Omary.

Naye  Mratibu wa CHF Wilaya ya Kongwa Amos Erenest amesema kuwa  wakina mama waliofika kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kliniki wamekuwa wakihamasishwa kujiunga na  Bima hiyo mwananchi akijiunga, kaya moja yenye watu sita kwa gharama ya shilingi elfu 30.

Pia Erenest ameongezea kwa kusema kuwakipindi mtu atakapo  jiunga  papo kwa papo anawezaa kuanza kupata matibabu kwa gaharama hiyo nafu.

“Hivyo ndugu zangu wananchi kama ilivyo kwa Sera ya Afya ya Serikali ya awamu ya Tano kwa kuwapenda watanzania wake  kuepukana na usumbufu wa matibabu ni vizuri tukawa na Bima hii ya Afya yenye gharama nafuu,  katika watu sita hao kila mmoja anakuwa na kitambulisho chake”, ametoa wito Erenest.

Kwa Upande wake mnufaika wa CHF iliyoboreshwa Neema Mazengo anasema kupitia Bima hiyo amekuwa akipata matibabu mazuri na sambamba na kupata dawa kwa bei nafuu tofauti na awali kabla ya kuwa na bima hiyo.

“Toka nijiunge na CHF mwezi wa pili nimekua nikija hapa kituoni na Napata matibabu vizuri tu,vipimo na dawa vyote Napata bure,kwa kweli imenisaidia sana yaani kuna utofauti mkubwa sana kwa sasa na kabla sijawa na kadi hii,niwasihi tu wananchi wengine ambao bado hawajakata Bima hii kwani ni gharama ndogo alafu unatibiwa wewe na watu wengine sita kwa mwaka mzima”ameeleza Mazengo.