Home Mchanganyiko JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA LA ENDELEA KUKOMESHA UHALIFU

JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA LA ENDELEA KUKOMESHA UHALIFU

0

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya gari iliyo fungwa taa kali,vimulimli na ving’ora katika magari yaliyokamatwa leo kwa kutokuwa na kibali cha kufunga vitu hivyo leo jijini Dodoma.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ndani ya gari lililobeba mzigo wa nyaya za umeme DRUM nne zenye ukubwa wa milimita 95 ABC zilizokamatwa jijini Dodoma.

…………………………………………………………

Na.Majid Abdulkarim, Dodoma

Jeshi Mkoani Dodoma limeendelea kufanya msako na kukamata wahalifu ambao wamekuwa wakijihusiaha na vitendo vya kihalifu huku likitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi hilo na kuwafichua watu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo hivyo.

Kauli hiyo imebainishwa leo na  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi Habari leo Jijini Dodoma.

Aidha Muroto amesema kuwa yamekamatwa magari 27 yaliyofungwa ving’ora, vimulimuli, taa zenye mwanga mkali na taa zenye kuwaka kwa kubadilisha rangi kwani magari pekee yanayoruhusiwa kisheria kufunga vimulimuli,ving’ora na kuwasha taa ni magari yanayofanya kazi za dharura kama magari ya polisi,majeshi,misafara ya viongozi,ya kubebea wagonjwa,ya zima moto na magari mengine yaliyopewa kibali maalumu na waziri mwenye dhamana kuruhusiwa kusafirisha mizigo yenye ukubwa unaozidi vipimo barabara.

‘’Ni marufuku kujiongezea taa kali,vimulimli na ving’ora katika magari yasiuoruhusishwa ni kosa kisheria , kila dereva azingtie sheria za barabarani wasifunge taa kali, wasigunge vimulimuli na ving’ora katika magari yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya usalama wa barabarani na kila dereva alinde uhai wake na watu wengine’’amesisitiza Muroto.

Katika hatua nyingine Muroto amesema kuwa wamekamata gari lililobeba mzigo wa nyaya za umeme DRUM nne zenye ukubwa wa milimita 95 ABC zinazokadiriwa kuwa urefu wa milimita elfu moja kila moja.

‘’Watuhumiwa wanasafirisha bila vibali wala risiti huku wakitumia mbinu ya kuficha nyanya hizo chini mizigo ya bidhaa nyingine za nyumbani kwenye gari hilo yaani nyaya zinasafirishwa kutoka mkoa wa Mwanza kwenda Dar es salaam’’ ameeleza Muroto

Naye Mhandisi wa Miradi ya REA awamu ya tatu Mkoani Dodoma Tumaini Mchonya amesema hujuma zilizofanyika ni kuwarudisha nyuma kimaendeleo kwani gari hilo kweli wamekuta lina DRUM 4 ambapo DRUM hizo za waya  hutumika kusambaza umeme kwa wananchi yaaani( LV Distribution Network) hupeleka umeme vijijini moja kwa moja na mjini hivyo walifu hao wameweka alama ya TANESCO/REA ili ionekane kama ndio utambulisha wake.

Kwa upande mwingine Muroto amesema kuwa Jeshi hilo pia limewakamata Joram Msigala (35) mkazi wa kijiji cha kiboriani wilayani mpwapwa kwa kosa la kulima Bhangi katika shamba lenye ukubwa wa robotatu, Issa Abdalaah (43) Dereva na mkazi wa Dar es salaam kwa kosa la kukutwa na gari ambalo alikuwa hana card wala umiliki wa gari hilo na kudhaniwa kuwa ni la wizi akisafirisha kutoka Dar es salaam kwenda kigoma na kumkamata Husein Ibrahim (35) mkazi wa Tabora kwa kukutwa na mabegi mawili ya Bhangi yenye ujazo wa kilogramu 35 akisafirisha kwenye basi la Simba Mtoto linalofanya safari zake kutoka Dodoma kwenda Tanga.