Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemai Jafo akiongea na Viongozi wapya walioteuliwa kushika nyadhifa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa leo kwenye Ofisi ya Rais- TAMISEMI iliyoko Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemai Jafo(kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mkuu wa Mkoa Mpya wa Dar es salaam, Mhe. Aboubakar Kunenge baada ya kuongea na Viongozi wapya walioteuliwa kushika nyadhifa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa leo kwenye Ofisi ya Rais- TAMISEMI iliyoko Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemai Jafo(kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Katibu Tawala wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Bi.Johari Khamis baada ya kuongea na Viongozi wapya walioteuliwa kushika nyadhifa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa leo kwenye Ofisi ya Rais- TAMISEMI iliyoko Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemai Jafo akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wapya walioteuliwa kushika nyadhifa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa leo kwenye Ofisi ya Rais- TAMISEMI iliyoko Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma
………………………………………………………..
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya kufanya kazi kwa kuwasaidia wananchi kwa kutatua kero na shida zao ili kuwawezesha kuleta maendeleo yatakayoinua uchumi.
Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dodoma alipokutana na viongozi hao wakati wa kuwakabidhi vitendea kazi na miongozo juu ya kutekeleza majukumu yao kikamilifu katika maeneo yao.
Mhe. Jafo amesema kuwa viongozi hao wanawajibu mkubwa wa kuwalinda wananchi kutopata matatizo na kuhakikisha wanainua uchumi wao na kuwaletea maendeleo.
Mhe. Jafo amesema kuwa viongozi hao wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanasimamia fedha kiasi cha shilingi billioni 170 zilizopelekwa katika mamlaka za serikali za mitaa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu katika mamlaka za serikali za mitaa.
“Ili kufanikiwa katika utendaji wenu lazima kuwa na mawasiliano mazuri na watendaji wenu, kufanya kazi kwa muda maalum na kufata kanuni , taratibu na sheria zilizopo katika kutimiza majukum yenu ili kuhakisha mnaleta utendaji mzuri katika maeneo ya kazi”, amesisitiza Mhe. Jafo
Lakini pia Mhe. Jafo aendelea kuwasisitiza viongozi hao kuheshimu mipaka ya majukumu yao na kuwa na ushirikiano wa kutosha kwa kila ngazi wanazofanya nazo kazi kwani lengo ni moja la kuleta ufanisi katika utendaji ambao matokeo yake ni kuleta maendelo kwa watanzania.
“Unapokuwa kiongozi sio lazima wewe uwe bora peke yako hata watendaji wako watakiwa kuwatengenezwa na wao kuwa bora ili kuleta chachu ya kuwa na watendaji bora nchini na kwa kufanya hivyo katika utendaji wenu mtakuwa mmeahacha alama kubwa katika taifa hili”, ameeleza Mhe. Jafo.
Kwa kuongezea Mhe. Jafo ametoa wito kwa viongozi hao kuhakikisha wanasimamia fedha za miradi zinazoletwa katika maeneo yao ya kazi, usimamizi wa wa mapato kahakikisha yanafika katika mfuko wa serikali na so vinginevyo.
“Hakikisheni watu wanaocheza na mifumo ya mapato kwa kukwepesha mapato yasiingie katika mfuko wa serikali wanachukuliwa hatua haraka sana kwani huo ni ubadhilifu”, amesema Mhe. Jafo
Naye Katibu Mkuu Ofis ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamuhanga amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii, weledi mzuri na kufata kanuni na sheria ili kuleta ufanisi katika utendaji kwa kusimamia fedha sinazoletwa na serikali katika maeneo yao zinatekeleza miradi iliyopangwa kwa ufasaha.
“Jukumu kubwa kwenu ni kusimamia mapato katika maeneo yenu na kuwa na matumizi mazuri ya ofisi na nafasi zenu kwani mmepewa dhamana na Mh. Rais”, ameeleza Mhandisi Nyamuhanga.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakari Kunenge akizungumza kwa niaba ya viongozi hao amesema kuwa hawata muangusha Mhe Rais kwa kuwa na ushirikiano wa karibu na watendaji wa TAMISEMI.
“Hivyo wenzangu sasa ni wakati wa kwenda kutekeleza maelekezo tuliyopewa na viongozi wetu kwa kufata nasaha walizotupatia kwa kushirikianan na watendaji wetu katika mamlaka za serikali za mitaa”, amesisitiza Kunenge.