Wachezaji wa Real Madrid wakiwa wamemuinua juu kocha wao, Mfaransa Zinedine Zidane baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Villarreal, mabao ya Karim Benzema dakika ya 29 akimalizia pasi ya Luka Modric na 77 kwa penalti Uwanja wa Alfredo Di Stéfano hivyo kutwaa taji la La Liga. Ushindi wa leo unaifanya Real Madrid ifikishe pointi 86 na kuwaacha mabingwa watetezi, Barcelona kwa pointi saba baada ya wote kucheza mechi 37 na hilo linakuwa taji la 34 la LaLiga kwa Real Madrid kihistoria na la pili kwa Zidane kama kocha PICHA ZAIDI SOMA HAPA