Wakati wagombea wa nafasi ya ubunge kupitia chama cha mapinduzi
wakichukuwa fomu kuomba ridhaa ya chama hicho kupeperusha bendera
ikiwa siku ya pili Leo huku wagombea wakifika 69 ndani siku
mbili.
Mvuto huo umekolezwa leo baada ya wakili maarufu Albert Msando
kuchukuwa fomu kuomba ridhaa ya wanachama kugombea nafasi hiyo kupitia
chama hicho ikiwa ni mlolongo wa wagombea akiwemo Philemon Mollel
Mrisho Gambo na Kalist Lazaro waliochukuwa jana.
Aidha katika nafasi ya viti maalum kupitia umoja wa wanawake UWT yupo
mwanadada maarufu Kabula Juma Sukwa ambaye ameonyesha njia kwa
wanawake wengine kuomba ridhaa hadi jioni ya leo zaidi ya kinamama 39
wamejitokeza kuomba nafasi hizo.
Duru za kisiasa mkoani hapa zinaonyesha kuwepo kwa kimuhemuhe na
wanachama wanakazi kubwa kuona nani ni nani kujua atapitishwa na chama
hicho kuopeperusha bendera kwenye bunge lijalo.
Hata hivyo mchuano utakuwa mkali kwa wagombea kutokana na wingi wao
kila moja akionyesha nia ya kutaka kuhudumia wananchi kupitia nafasi
za ubunge ndani ya chama hicho kikongwe nchini.